Advertisements

Friday, October 7, 2016

MAADHIMISHO YA FIMBO NYEUPE YAFANA JIJINI MBEYA.

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Ackso Mwansasu akihutubia katika kilele cha maadhimisho ya siku ya Fimbo nyeupe duniani ambayo kitaifa yamefanyika jijini Mbeya.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akitoa salamu za mkoa wa Mbeya katika kilele cha maadhimisho ya siku ya Fimbo nyeupe duniani ambayo kitaifa yamefanyika jijini Mbeya.
Mwenyekiti wa Chama cha Wasioona Tanzania(TLB), Luis Benedicto akitoa salamu za Chama katika kilele cha maadhimisho ya siku ya Fimbo nyeupe duniani ambayo kitaifa yamefanyika jijini Mbeya
Katibu wa TLB Tawi la Temeke, Protas Mutakyanga akisoma risala ya Chama cha wasioona katika kilele cha maadhimisho ya siku ya Fimbo nyeupe duniani ambayo kitaifa yamefanyika jijini Mbeya.
Katibu Mkuu wa Chama cha Wasioona Tanzania, Emmanuel Saimon akitoa utambulisho kwa wanachama wake katika kilele cha maadhimisho ya siku ya Fimbo nyeupe duniani ambayo kitaifa yamefanyika jijini Mbeya.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Ackso Mwansasu akiangalia baadhi ya bidhaa za wajasiliamali wasioona katika kilele cha maadhimisho ya siku ya Fimbo nyeupe duniani ambayo kitaifa yamefanyika jijini Mbeya.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Ackso Mwansasu akiongozwa na Afisa maendeleo ya jamii Mkoa wa Mbeya kutembelea baadhi ya mabanda ya wajasiliamali katika kilele cha maadhimisho ya siku ya Fimbo nyeupe duniani ambayo kitaifa yamefanyika jijini Mbeya.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Ackso Mwansasu awa sambamba na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mbunge Viti maalum Mkoa wa Mbeya Dk. Mary Mwanjelwa kushuhudia baadhi ya bidhaa za wajasiliamali katika kilele cha maadhimisho ya siku ya Fimbo nyeupe duniani ambayo kitaifa yamefanyika jijini Mbeya.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Ackso Mwansasu akisikiliza maelezo kutoka kwa mjasiliamali katika kilele cha maadhimisho ya siku ya Fimbo nyeupe duniani ambayo kitaifa yamefanyika jijini Mbeya.
Baadhi ya Viongozi wakifuatilia matukio mbali mbali katika sherehe za fimbo nyeupe.Viongozi wa meza kuu wakiwa katika maadhimisho ya siku ya fimbo nyeupe.
Mc Charles Mwakipesile akiendesha ratiba ya maadhimisho ya siku ya fimbo nyeupe iliyofanyika kitaifa jijini Mbeya.
CHAMA cha Wasioona Tanzania (TLB) kimeungana na wananchi wote duniani kuadhimisha siku ya fimbo nyeupe katika sherehe zilizofanyika kitaifa jijini Mbeya.

Aidha maadhimisho hayo ambayo mgeni rasmi alikuwa ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Ackson Mwansasu yalipambwa na burudani mbali mbali ukiwemo mpira na nyimbo kutoka kwa waioona.

Dk. Tulia Mwansasu ametoa wito kwa Jamii na Taasisi mbali mbali nchini zimetakiwa kuhakikisha zinajenga miundombinu rafiki itakayowawezesha watu wenye ulemavu kupata huduma kama watu wengine kwa mujibu wa Sheria ya walemavu namba 9 ya mwaka 2010.

Naibu Spika alisema Walemavu wanakumbwa na changamoto mbali mbali lakini kubwa ni miundombinu ya kuwawezesha kufikia malengo yao ikiwemo kukosa nafasi ya kuingia katika baadhi ya majengo marefu.

Alisema ni vema miundombinu mbali mbali ikaboreshwa na kujengwa kwa kuzingatia usawa kwa wote hususani miundombinu katika Shule ili kuwawezesha watoto wenye ulemavu kupata elimu kama wengine.

Alisema Serikali inajitahidi kuboresha miundombinu mbali mbali kama Wizara ya Afya ambayo inakamilisha utaratibu wa upatikanaji wa Bima ya afya kwa wote wakiwemo wenye ulemavu ili wapate matibabu vizuri.

Aliongeza kuwa Wizara ya Elimu pia inaandaa muongozo wa elimu jumuishi ikiwa ni sambamba na kuhakikisha inafufua vyuo vya ufundi ambavyo vilikuwepo kwa lengo la kuwawezesha wenye ulemavu kupata elimu ya ufundi.

Awali akisoma Risala ya Chama cha Wasioona Tanzania (TLB), Protas Mutakyanga katibu wa TLB Tawi la Temeke kwa niaba ya Katibu Mkuu alisema hivi sasa Tanaznia ina wasioona zaidi ya 35,000 ambao wanakabiliwa na changamoto nyingi.

Alizitaja changamoto hizo kuwa ni pamoja na miundombinu rafiki ya kuwawezesha kutembea, ufutwaji wa ruzuku ya kuweza kukiendesha chama,kufungwa kwa vyuo vya ufundi jambo lililopelekea kukosa ujuzi, mifumo duni ya upatikanaji wa mikopo na usumbufu wa upatikanaji wa matibabu.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Wasiiona Tanzania (TLB) Luis Benedicto, aliipongeza Serikali ya awamu ya nne na awamu ya tano kwa kujali watu wenye ulemavu kwa kuwatengenezea mazingira rafiki ya upataji wa ajira.

Mwenyekiti huyo alipongeza uteuzi wa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria, Amos Mpanju ambaye ni mlemavu wa macho pamoja na uteuzi wa Naibu Waziri wa Afya Dk. Abdalah Possi ambaye ni mlemavu wa ngozi.

Akimkaribisha mgeni rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amosi Makalla alisema Mkoa wa Mbeya pekee una watu wasioona 603 ambao serikali yake imekuwa ikishirikiana katika kutatua changamoto zinazowakabili.

Aidha aliiomba jamii kuwa na upendo kwa watu wenye ulemavu kwa kuwa hakuna aliyependa kuzaliwa kuwa mlemavu ili hali wengine wameupata ukubwani.

“Hakuna aliyependa kuzaliwa awe mlemavu ni mapenzi ya Mungu hivyo tusiwanyanyapae ni binadamu wenzetu kwani hata sisi ni walemavu watarajiwa maana hatujui ya mbeleni” alisema Makalla.

MBEYA YETU

No comments: