Advertisements

Sunday, October 2, 2016

MAAFISA WATATU WA SERIKALI WATEKETEZWA KWA MOTO DODOMAPicha ya Mtandao.
By Mwandishi Wetu, Mwananchi

Dodoma. Watu watatu wakiwamo watafiti watatu na dereva wa Kituo cha Utafiti wa udongo na maendeleo ya ardhi Seliani mkoani Arusha wameteketezwa kwa moto wilayani Chamwino mkoani Dodoma.

Katika tukio hilo lililotokea jana saa 12:30 jioni katika Kijiji cha Iringa Mvumi, gari walilokuwa wanatumia aina ya Toyota Hilux mali ya kituo hicho, lilichomwa moto.

Kabla ya kuchomwa moto, watafiti hao mmoja kati yao mwanamke, walivamiwa na wanakijiji cha Iringa Mvumi waliwakatakata kwa mapanga na silaha za jadi kisha kuwachoma moto hadi kufa.

Kamanda wa Polisi Mkoani Dodoma, Lazaro Mambosasa amethibitisha hilo na akasema atatoa taarifa za tukio hilo baadaye.

Taarifa za awali zilizopatikana zimesema chanzo cha tukio hilo ni mwanamke mmoja wa kijijini hicho kupiga yowe kuashiria kwamba ameona watu ambao anahisi ni wanyonya damu (mumiani).

Taarifa hizo zilipofika kijijini, ndipo wanakijiji wakaenda kuchoma gari na kuwaua na kuwachoma moto.

Baada ya tukio hilo, Polisi walituma makachero na Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) walifika kijijini hapo na kuanza msako mkali.

Miili ya marehemu imehifadhiwa katika chumba cha maiti Hospitali ya Mvumi.

1 comment:

Anonymous said...

BADO TUPO NYUMA SANA TANZANIA....MJI WETU MKUU WANACHOMWA BINADAMU WASIO NA MAKOSA, HUKO MWANZA NA SHINYANGA WANAUAWA WATOTO, WATU WENYE ALBINISM NA WAZEE. SERIKALI NA MEDIA NYINGI ZINAENDELEA KUTOWAPA ELIMU WANANCHI KUTOAMINI MAMBO YA UNYONYAJI DAMU (HAYO MAMBO NI MAPOKEO TU NA WALA HAYANA UKWELI HATA KIDOGO) LAKINI HAKUNA ELIMU WALA KUKANUSHA HUO UJINGA KUTOKA SERIKALINI. MAGAZETI PIA YANAAMINISHA WANANCHI KUWA KUNA MAMBO HAYO. WALIOFANYA HAYO WANATAKIWA WANYONGWE TU HAKUNA MTU MWENYE MAMLAKA YA KUTOA ROHO ZA WENGINE.