Advertisements

Saturday, October 29, 2016

Majibu ya Ubalozi wa Marekani kwa Tamko la Wizara ya Afya la Oktoba 25

Image result for usa flag
Ubalozi wa Marekani
Dar es Salaam
TANZANIA

27 Oktoba, 2016
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


Majibu ya Ubalozi wa Marekani kwa Tamko la Wizara ya Afya la Oktoba 25

Dar es Salaam, TANZANIA. Marekani inathamini kwa kiasi kikubwa ushirikiano wake wa muda mrefu na wenye mafanikio na nchi ya Tanzania katika sekta ya afya, hususan maendeleo ambayo Tanzania imeyapata katika mwitikio wake duniani kuhusu maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) na Ukimwi chini ya ufadhili wa Mpango wa Rais wa Marekani wa Kukabiliana na UKIMWI (PEPFAR).  Tumedhamiria kufanya kazi na Tanzania katika kukabiliana na janga la VVU/UKIMWI kwa ujumla na kwa hivyo basi, tumelipokea tamko la Oktoba 25 la Mheshimiwa Waziri Ummy Mwalimu, ambalo limesisitiza dhamira ya serikali ya Tanzania kutoa huduma ya afya na VVU kwa raia wa Tanzania wote bila ubaguzi.  Pia, tunaishukuru serikali ya Tanzania kwa kukubali viwango vya shirika la afya duniani (WHO) na taratibu zinazokubalika kimataifa katika kinga na tiba, pamoja na mwongozo wa kutoa huduma kwa Makundi Maalum.  Dhamira ya wazi ya waziri kufanya kazi na washirika, pamoja na mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) yanayoisaidia serikali ya Tanzania katika eneo hili itasaidia kuhakikisha huduma zinawafikia watu na sehemu zinakohitajika zaidi, ikiwa ni pamoja na takriban wanaume, wanawake na watoto milioni 1.4 wanaoishi na VVU/UKIMWI nchini kote. Serikali ya Marekani inaunga mkono mwendelezo wa ushirikiano huu na Tanzania katika kukabiliana na majukumu ya kiafya nchini, pamoja na lengo letu la pamoja la Kizazi Huru dhidi ya maambukizi ya UKIMWI.


Kwa taarifa zaidi kuhusu hafla hii, tafadhali wasiliana kwa barua pepe na Japhet Sanga (SangaJJ@state.gov), Afisa Habari Mwandamizi wa Ubalozi wa Marekani, Dar es Salaam.

No comments: