Advertisements

Saturday, October 29, 2016

MWAMKO MDOGO WA USHIRIKI WA WANANCHI SIKU YA USAFI KITAIFA MKOANI MOROGORO

Kaimu Mkurugenzi Idara ya Mazingira Bwana Richard Muyungi akiwa katika Manispaa ya Morogoro kata ya Kihonda,  akishiriki kufanya usafi katika siku ya jumamosi ya mwisho wa mwezi ambayo ni siku ya usafi kwa Tanzania nzima.
Sehemu ndoogo ya idadi ya Wananchi wa Manispaa ya Morogoro waliojitokeza kushiriki katika siku ya usafi wa mazingira ya kila jumamosi ya mwisho wa mwezi  iliyofanyika katika kata ya Kihonda. Wananchi wengi wamelalamika kutokuwa na elimu juu ya siku hiyo ya usafi
.
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Mazingira Bwana Richard Muyungi akiwa katika Manispaa ya Morogoro kata ya Kihonda,  akishiriki kufanya usafi katika siku ya jumamosi ya mwisho wa mwezi ambayo ni siku ya usafi kwa Tanzania nzima.
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Mazingira Bwana Richard Muyungi akitoa maagizo juu ya kuhamasisha Wananchi juu ya kushiriki katika siku ya usafi juamosi ya mwisho wa mwezi,  kwa Afisa Afya wa Mkoa wa Morogoro Bwana Simon Malulu na Afisa Afya na Mazimgira wa Wilaya Bwana Amri Ugumba

Serikali  ya Mkoa  wa Morogoro imeagizwa kufuata maagizo ya Serikali kuwa kila jumamosi ya mwisho wa mwezi kuwa  ni siku ya kufanya usafi  wa mazingira. Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais, Richard Muyungi aliposhiriki kufanya usafi wa siku ya jumamosi  ya mwisho wa mwezi  katika Manispaa ya Morogoro .
Tukio hilo limehudhuriwa na  Watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Manispaa ya Morogoro na idadi ndogo sana ya Wananchi. Akiongea katika eneo la tukio  mkurugenzi  Muyungi amesema kuwa amesikitishwa sana na    Wananchi kutokuwa na elimu ya kushiriki katika swala zima la usafi wa mazingira na wala kutokuonyesha  kuwa na uelewa wowote juu ya siku ya usafi Kitaifa.
‘Kwa kweli nimesikitishwa sana na hali hii nilioona leo Wananchi hawana uelewa kabisa juu ya suala zima la siku ya usafi na wala  hawajui nini kinachoendelea juu ya usafi’ alisema Muyungi. Mkoa wa Morogoro bado upo nyuma sana kwenye kuzingatia siku ya usafi na haya elimu ya usafi  kwa wananchi wake bado haijawaingia.
Wakiongea mbele ya Bwana Muyungi, Afisa Afya wa Mkoa Bwana Simon Malulu na Afisa Afya na Mazingira wa Manispaa Bwana Amri Ugumba  wamekiri kuwa mwamko wa ufanyaji wa usafi kwa siku hii ya leo ni mdogo san. Wananchi bado hawana uelewa mkubwa juu ya siku hiyo. Wameahidi kuanza kufanyia kazi suala hilo na pia kuanza kuchukua hatua kwa wote watakaopuuzia siku ya usafi ambayo ni juamosi ya mwisho wa mwezi.
Ofisi ya Makamu  Rais ni MRatibu wa masuala yote ya Mazingira hivyo basi hutembelea na kufuatilia kwa ukaribu kujua Mikoa mbalimbali wanavyosimamia masuala ya utunzaji wa mazingira na usafi kwa ujumla. 

No comments: