Advertisements

Sunday, October 2, 2016

UKAWA waja na Maazimio 8 ya kukabiliana na Prof. Lipumba na Msajili wa vyama

Umoja wa Katiba ya Wananchi umedhamiria kwenda mahakamani kumshtaki Prof. Lipumba na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini kutokana na mgogoro unaoendelea ndani ya Chama cha Wananchi (CUF).

Katika kikao walichofanya jana, UKAWA walipitisha maazimio kukabiliana na mgogoro unaoendelea ndani ya CUF. Maazimio hayo ni pamoja na;-
  1.  Hatumtambui Prof. Lipumba kama mwanachama wa CUF na Mwenyekiti mwenza wa UKAWA
  2.  UKAWA wanautambua uongozi wa Julius Mtatiro na Maalim Seif
  3.  Wanachama wa vyama vinavyounda UKAWA wasitoe ushirikiano kwa Prof. Lipumba na washirika wake
  4.  Wenyeviti wa mitaa, vijiji, Madiwani, Wabunge wasitoe ushirikiano kwa Prof. Lipumba na washirika wake
  5.  Wabunge wote wanaomuunga mkono Prof. Lipumba  watatimuliwa ndani ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni
  6.  Ushirikiano wa kisiasa Tanganyika na Zanzibar utashughulikiwa na UKAWA
  7.   Mawakili wa UKAWA watamfunguliwa mashtaka Msajili wa Vyama vya Siasa nchini kwa matumizi mabaya ya madaraka na
  8.  Mawakili wa UKAWA watamfungulia mashtaka Prof. Lipumba.
Kwa upande wake Prof. Lipumba aliwataka wanachama wa CUF kuwa wamoja na kusema kuwa yeye hajali kuhusu UKAWA kikubwa anachoangala ni kuijenga upya CUF.

1 comment:

Anonymous said...

kamasio kiongozi wa cuf huna haki ya kusema haumtambui lipumba,utakuwa unaeneza siasa za kibaguzi ndani ya chama kingine,waache wenyewe watatue mgogolo wao,wewe fuata katiba ya chadema!cuf ni chama kina wanachama wake,viongozi wake,na katika mgogolo wao,kuna wanaotaka lipumba awe mwenyekiti,na wengine hawataki.waachiwe wanacuf wenyewe pamoja na waasisi wao ili watatue mgogolo wao wenyewe,na sio chadema!NI DHAMBI KUBWA CHADEMA KUSEMA HAWAMTAMBUI