Advertisements

Wednesday, October 19, 2016

WAWAKILISHI WA WANAWAKE WALIOPANDA MLIMA KILIMANJARO NA KUWEKA MAAZIMIO YAO WAZUNGUMZA NA VYOMBO VYA HABARI LEO

Kijana wa Kitanzania aliyekuwa kwenye msafara wa Kilimanjaro, Judith Severin (wa pili kutoka kulia) akisoma tamko kuhusu yaliyojadiliwa katika kongamano la wanawake ambao ni wakulima wadogo wadogo waliokuwa kujadili changamoto na kutoka na maadhimio hasa katika suala la kumiliki Ardhi.
Mkurugenzi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania TGNP Bi Lilian Liundi akizungumza na waandishi wa habari kuhusu walivyowasimamia wanawake wa Tanzania waliowawakilisha wenzao katika kongamano la wanawake lililiofanyika Mkoani Kilimanjaro.
Mwanamke aliyefika kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro, Flola Matiasi  akizungumza na vyombo vya habari kuhusu alivyofanikiwa kufika katika kilele cha mlima Kilimanjaro na kusimika maadhimio katika kilele cha mlima huo hasa umiliki wa ardhi kwa wanawake.
Maneja wa Programu ya Ushawishi na Utetezi, Grace Kisetu akitoa ufafanuzi wa swali lililoulizwa na mwandishi wa habari katika mkutano uliofanyika leo katika ukumbi wa TGNP Mtandao.
Meneja Kilimo na Haki ya Ardhi kutoka Action Aids , Elias Mtinda akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mchango Action Aids katika kupigania haki za wanawake hapa nchini Tanzania.
Baadhi ya wanawake waliowawakilisha wenzao katika Kongamano lililofanyika Mkoani Kilimanjaro na kuwakutanisha wanawake kutoka nchi mbalimbali barani Afrika.

No comments: