ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, November 1, 2016

KAMPUNI YA MANTRA TANZANIA IMETOA MSAADA WA VIFAA VYENYE THAMANI YA MILIONI 12 KWA DAWATI LA KIPOLISI LA KUSHUGHULIKIA MASUALA YA UKATILI WA KIJINSIA NA WATOTO.

 Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Dkt Binilith Mahenge akipokea msaada wa Vifaa kutoka kwa Afisa Mahusiano wa kampuni ya Mantra Tanzania Khadija Pallangyo.

Kampuni hiyo inajihusisha na utafiti wa uchimbaji wa Madini aina ya Uranium katika eneo la Mto mkuju wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma , imekabidhi msaada wa vifaa mbalimbali vya ofisi kwenye Ofisi ya Dawati la kipolisi la Kushughulikia masuala ya ukatili wa Kijinsia na watoto mjini Songea mkoani RUVUMA vikiwa na thamani ya shilingi milioni 12.

No comments: