ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, November 26, 2016

MHANDISI HAMAD MASAUNI AZINDUA KAMPENI YA ABIRI PAZA SAUTI KITUO KUU CHA MABASI, UBUNGO JIJINI DAR ES SALAAM

 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kushoto) akikata utepe ikiwa ni ishara ya kuzindua Kampeni ya Abiria Paza Sauti ndani ya basi la Machame Express katika Kituo Kikuu cha Mabasi, Ubungo jijini Dar es Salaam leo.Kampeni hiyo iliandaliwa na Mabalozi wa RSA kwa kushirikiana na Taasisi mbalimbali nchini. Kushoto ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga.Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na abiria mara baada ya kuzindua Kampeni ya Abiria Paza Sauti katika Kituo Kikuu cha Mabasi, Ubungo jijini Dar es Salaam. Masauni aliwataka abiria nchini kutoa taarifa kwa haraka pindi wanapoona dereva anavunja sheria na pia kila abiria ni wajibu wake kujua haki zake. Kushoto niMlezi wa RSA Taifa ambaye pia ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akigawa vipeperushi vya Kampeni ya Abiria Paza Sauti, kwa abiria wa Basi la Machame Express katika Kituo Kikuu cha Mabasi, Ubungo jijini Dar es Salaam mara baada ya Naibu Waziri huyo kuizindua Kampeni hiyo ambayo iliratibiwa na Mabalozi wa Usalama Barabarani (RSA) kwa kuzishirikisha Taasisi mbalimbali nchini.Kushoto niMlezi wa RSA Taifa ambaye pia ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kulia) akimsikiliza Katibu wa Mabalozi wa Usalama Barabarani(RSA) Taifa, Asina Omary  alipokuwa anatoa historia ya RSA pamoja na majukumu yake kabla ya Naibu Waziri huyo kuzindua Kampeni ya Abiria Paza Sauti katika Kituo Kikuu cha Mabasi, Ubungo jijini Dar es Salaam leo. Kampeni hiyo iliratibiwa na Mabalozi wa RSA kwa kushirikiana na Taasisi mbalimbali nchini. 


Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na wananchi katika Kituo Kikuu cha Mabasi, Ubungo jijini Dar es Salaam mara baada ya kuzindua Kampeni ya Abiria Paza Sauti iliyoratibiwa na Mabalozi wa Usalama Barabarani (RSA) nchini wakishirikiana na Taasisi mbalimbali nchini. Katika hotuba yake, Masauni aliwataka abiria nchini kutoa taarifa kwa haraka pindi wanapoona dereva anavunja sheria na pia ni wajibu wa kila abiria kujua haki yake. Kulia niMlezi wa RSA Taifa ambaye pia ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga. Kushoto ni Katibu wa Mabalozi wa Usalama Barabarani(RSA) Taifa, Asina Omary. 
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kushoto) akienda kuzindua Kampeni ya Abiria Paza Sauti na Mabalozi wa Usalama Barabarani nchini (RSA) ndani ya Kituo Kikuu cha Mabasi, Ubungo jijini Dar es Salaam. Masauni alizindua Kampeni ya Abiria Paza Sauti iliyoratibiwa na Mabalozi wa RSA kwa kushirikiana na Taasisi mbalimbali nchini. Watatu kushoto ni Mlezi wa RSA Taifa ambaye pia ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akimsalimia Katibu wa Mabalozi wa Usalama Barabarani(RSA) Taifa, Asina Omary (kulia), alipokuwa anawasili Kituo Kikuu cha Mabasi, Ubungo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuzindua Kampeni ya Abiria Paza Sauti iliyoandaliwa na Mabalozi wa RSA na kushirikisha Taasisi mbalimbali nchini. Kushoto niMlezi wa RSA Taifa ambaye pia ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga.

No comments: