ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, November 26, 2016

MWIGULU NCHEMBA MGENI RASMI MAHAFALI YA 42 YA CHUO CHA USIMAMIZI WA FEDHA (IFM)

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akisalimiana na Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Chuo cha Usimamizi wa Fedha nchini (IFM) Bi. Juliana H. Lema wakati alipowasili chuoni hapo kwaajili ya maandalizi ya kuelekea katika mahafali ya 42 ya chuo hicho yaliyofanyika katika viwanja vya Karemjee jijini Dar es Salaam. Wa pili kushoto ni Mkuu wa Chuo hicho Profesa Taadeo Andrew Satta na mwenye miwani ni Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Elisante Ole Gabriel.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, akisalimiana na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Elisante Ole Gabriel, wakati alipowasili chuoni hapo kwaajili ya msafara wa kuelekea katika mahafali ya 42 ya chuo hicho yaliyofanyika katika viwanja vya Karemjee jijiniI Dar es Salaam. Aliyenyoosha mkono ni Mkuu wa Chuo hicho Profesa Taadeo Andrew Satta akifuatiwa na Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Chuo cha Usimamizi wa Fedha nchini (IFM) Bi. Juliana H. Lema.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (mwenye kofia nyekundu), ambaye pia alikua ni mgeni rasmi katika Mahafali ya 42 ya chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) akiwa na Mkuu Wa Chuo hicho Profesa Taadeo Andrew Satta, (mwenye kofia nyeusi) wakiwa wako tayari kwaajili ya kuanza msafara wa kuelekea katika viwanja vya Karemjee jijini Dar es Salaam kwaajili ya ufunguzi wa mahafali hayo ya achuo hicho.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (mwenye kofia nyekundu), ambaye pia alikua ni mgeni rasmi katika Mahafali ya 42 ya chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) akiwa katika Msafara wa kelekea katika viwanja vya Karemjee jijini Dar es Salaam yalikofanyika Mahafali hayo ya chuo hicho mwishoni mwa wiki. Mwenye kofia nyekundu ni Mkuu wa Chuo hicho Profesa Taadeo Andrew Satta.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu, akiimba wimbo wa Taifa pamoja na Uongozi Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) waati wa mahafali ya 42 ya chuo hicho yaliyofanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya Karemjee jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa Baraza la chuo hicho Bi. Lettice K. Rutashobya., wa tatu ni kuu wa Chuo hicho Profesa Taadeo Andrew Satta akifuatiwa na Mkuu wa Kitivo cha Uhasibu, Benki na Fedha wa Chuo hicho Dkt. Mnzava.
Mgeni rasmi katika katika Mahafali ya 42 ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) nchini, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akizungumza na wahitimu wa ngazi mbalimbali wa chuo hicho (hawako pichani) katika viwanja vya Karemjee jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki hii.
Mgeni rasmi katika Mahafali ya 42 ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) nchini, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akimpongeza Rehema Sibuga mhitimu mmoja kati ya wahitimu wengine waliofanya vizuri zaidi katika miaka yote masomo yao chuoni hapo.
Mgeni rasmi katika Mahafali ya 42 ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) nchini, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba pamoja na uongozi Mkuu wa CHuo hicho wakitoa makofi ya pongezi kwa wahitimu wa ngazi mbalimbali waliofanikiwa kuhitimu. Mahafali hayo yalifanyika katika viwanja vya Karemjee jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

No comments: