Advertisements

Tuesday, November 15, 2016

Mtanzania aweka historia shindano la upishi MarekaniFredy Uisso
By Harriet Makweta, Mwananchi

Dar es Salaam. Mtanzania Fredy Uisso aliyekwenda Alabama, Marekani,kushiriki mashindano ya upishi ameibuka mshindi wa nne katika mashindano hayo ya kidunia.

Usiku wa kuamkia leo, Mkurugenzi Mtendaji wa World Food Championships Mike Mc Cloud, alimtangaza Uisso kuwa mshindi wa nne katika shindao hilo.

Uisso anaandika historia ya kuwa Mwafrika wa kwanza kuchaguliwa kushiriki fainali za mashindano hayo na kuibuka kuwa mshindi wa nafasi hiyo huku akiwabwaga wapishi 21 kutoka hoteli kubwa na maarufu duniani walioshiriki fainali hizo zilizoanza Novemba 8 mwaka huu.

No comments: