Siku chache zilizopita baada ya Wizkid kushinda tuzo hiyo, kulitokea sintofahamu huku mashabiki wa kiba wakiponda mchakato mzima wa utoaji tuzo huo ambapo website ya MTV EMA ilionesha kura zilionesha kuwa ni Alikiba ndiye aliyeshinda.
MTV EMA kupitia akaunti yao ya twitter wamethibitisha kumpa ushindi huo Alikiba ambapo yeye ameupokea kwa furaha sambamba na mashabiki wake.
Amesema baada ya mashabiki wake kulalamika kuhusiana na mkanganyiko huo, MTV EMA walifuatilia na kukiri kuwa na makosa na kuutumia ujumbe uongozi wake kuwa Alikiba ndiye mshindi halali, na sio Wizkid.
“Sasa ndio nimepata confirmation kwamba ni kweli tuzo inakuja Tanzania na vile vile mimi siwezi kuzungumzia, nitasubiri mpaka nizishike,” amesema Kiba.
Muimbaji huyo amedai kuwa habari hizo amezipokea kwa furaha kubwa na kuwashukuru mashabiki wake kwa kumwezesha kushinda na kuwa nyuma yake.
Wakati hup huo Kiba amempongeza Wizkid kwa ushindi wa tuzo nyingine ya Afrima. Kwa upande wa Wizkid, tayari amefuta post zote za Instagram alizokuwa ameweka kushangilia ushindi huo.
WALICHOKIANDIKA MTV EMA
GPLCongratulations to @OfficialAliKiba for his well-deserved win as Best African Act at the 2016 #MTVEMA
No comments:
Post a Comment