Advertisements

Sunday, November 27, 2016

SERIKALI YAMPOKONYA SUMAYE SHAMBA LAKE LENYE UKUBWA WA HEKTA 33

Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye amepokonywa na Serikali shamba lake lenye ukubwa wa hekta 33 kwa kile kilichoelezwa kushindwa kuliendeleza.

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi amesema kuwa Serikali imefikia uamuzi huo baada ya Sumaye kushindwa kuliendeleza kama notisi ya siku 90 ilivyoeleza.

“Oktoba 28, mwaka huu. Rais John Magufuli alibatilisha hati ya kumiliki ardhi ya shamba namba 3074 lililopo Mabwepande. Shamba hili lilikuwa na hati namba 53086. Jina la mmiliki lililoandikwa katika hati ni Frankline Sumaye,” amesema Hapi.

Sumaye ambaye alikuwa ni mmoja wa wasemaji tegemeo katika mikutano ya kampeni ya Uchaguzi Mkuu uliopita ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), anamiliki mashamba makubwa yaliyoko Morogoro na Mabwepande Dar es Salaam.

Baada ya Rais Magufuli kubatilisha hati hiyo, Hapi amesema kuanzia sasa ni marufuku kwa Sumaye kujihusisha na shamba hilo.

Kwa sababu hati yake imeshabatilishwa na akibainika kufanya chochote vyombo vya dola vitachukua nafasi yake.

“Vyombo vya ulinzi na usalama watakuwapo kwa ajili ya kuhakikisha kwamba shamba hili halitafanyiwa shughuli zozote, isipokuwa baada ya taratibu za manispaa zitakapofanyika,” amesisitiza Hapi.

Amesema amemwagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Kinondoni, Aron Kagurumjuli kupima viwanja vya shamba hilo na kwamba wananchi waliokuwa na mgogoro wa shamba hilo wafikiriwe.

Februari 5 mwaka huu, akiwa Morogoro, Rais John Magufuli aliwataka watu wote waliotelekeza mashamba kuyaendeleza, la sivyo atawanyang’anya na kuwapa wananchi.

4 comments:

Anonymous said...

Hii serikali inanyanyasa wananchi wake wazawa. It is very sad indeed.

Anonymous said...

Walipokuwa kwenye madaraka walijisahau wakaacha kurekebisha sheria ya ardhi. Sasa mambo yanawageukia. Kwa hii serikali ya sasa, sijui tunakwenda wapi. Kunyanganyana mashamba? Mwananchi mwaafrika ataishia kuwa kama mtumwa.

Anonymous said...

Ni sawa kabisa serikali inavyofanya hivyo sababu watu walijisahau na kujichukulia ardhi watakavyo bila ya kuendeleza sababu walikuwa madarakani kama sumaye na wenzake wengine,Sheria inasema ukipewa shamba ni lazima uliendeleze na siyo kuliacha kuwa pori kama hivyo sumaye alivyoliacha shamba lake hadi wananchi wakalivamia na kujenga nyumba zao hapo,sasa wanyonge walioingia hapo na kujenga nyumba zao ni lazima wafikirie na wapewe vipande vyao hapo vya ardhi.Sheria ni msumeno.

Anonymous said...

Sheria ni msumeno hakuna kuishi kwa kuogopa majina ya watu. Yale maisha ya "unajua mimi ni nani" yaliondoka na JK.