Advertisements

Monday, November 28, 2016

Tanzania na Zambia Kuimarisha TAZARA na TAZAMA

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza mazungumzo na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Zambia Edgar Lungu (aliyekaa) leo Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Lungu akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza mazungumzo na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri wa TanzaniaDkt. John Pombe Joseph Magufuli (aliyekaa) leo Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Mambo ya Nje ya Nchi na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Dkt. Augustine Mahiga (kushoto) pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Zambia wakisaini makubaliano ya kuwa na Mashauriano ya Kidiplomasia leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Mambo ya Nje ya Nchi na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Dkt. Augustine Mahiga (kushoto) pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Zambia wakionyesha mikataba ya makubaliano ya kuwa na Mashauriano ya Kidiplomasia iliyotiwa saini leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Waziri wa Nishati na Madini wa Tanzania Mhe. Profesa Sospeter Muhongo mara baada ya kumaliza mazungumzo na waandishi wa habari akiwa na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Zambia Edgar Lungu (nyuma mwenye tai nyekundu) leo Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Tanzania Balozi John Kijazi mara baada ya kumaliza mazungumzo na waandishi wa habari akiwa na mgeni wake Rais wa Zambia Edgar Lungu (hayupo pichani) leo Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na mgeni wake Rais wa Zambia Edgar Lungu (mwenye tai nyekundu) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi kutoka Tanzania na Zambia leo Ikulu jijini Dar es Salaam. Picha zote na: Frank Shija – MAELEZO.
  

Na. Immaculate Makilika – MAELEZO
SERIKALI za Tanzania na Zambia zimeahidi  kuimarisha  utendaji kazi wa reli ya TAZARA  na mradi  wa bomba la mafuta la TAZAMA yanayoendeshwa kwa ushirikiano wa  baina ya nchi hizo.
Akizungumza  leo,  Ikulu Jijini Dar es Salaam, Rais wa Zambia Mheshimiwa Edgar Lungu  alisema kuwa Tanzania na Zambia zitaendelea  kushirikiana kuiboresha  reli hiyo ili iweze kufanya kazi  kwa ufanisi.
Kwa upande Rais John Pombe Magufuli alisema reli  ya TAZARA na bomba la mafuta la TAZAMA zinakabiliwa na changamoto za mtaji na uongozi na hivyo kufanya reli hiyo kuwa na uwezo wa kusafirisha mizigo tani 128,000 tu, ambapo ilipoanzishwa mwaka 1976 ilikua na uwezo wa kubeba mizigo tani 500,000.
Ili kutatua changamoto hizo Rais Magufuli alisema kuwa “tumekubaliana kubadilisha  menejimenti ya TAZARA, kubadilisha sheria ili kuwezesha menejimenti hiyo kuongozwa na  mtu mwenye uwezo  ambaye si lazima awe anatoka Tanzania au Zambia”.
“Nia ya Serikali hizi ni kuongoza reli hiyo kibiashara  kwa maslahi na maendeleo ya nchi zote mbili” alisema Rais Magufuli.
Kwa mujibu wa Rais Magufuli malengo ya Serikali zote mbili ni kupunguza ucheleweshaji mizigo  kufika nchini Zambia, ambapo wamekusudia  kupunguza vituo vya kukagua magari ya mizigo hadi kufikia vinne.
Rais Magufuli alisema mbali kujenga kituo kimoja cha forodha huko Tunduma, ambapo kwa upande wa Zambia tayari wameshajenga kituo hicho na kwa upande wa Tanzania wanatarajia kujenga kituo chake  baada  ya mwaka mmoja na nusu kutoka sasa.
Sambamba  na hayo Serikali hizi mbili zimesaini makubaliano ya kuwepo kwa mashaurinao ya kidiplomasia, pamoja na kuahidi kuendeleza ushirikiao wa kihistoria baina ya nchi hizi mbili.

No comments: