Mtandao huu umefunga safari mpaka nyumbani kwa marehemu Sitta maeneo ya Masaki, jijini Dar es Salaam na kushuhudia baadhi ya viongozi wa vyama na serikiali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda wakifika kuwapa pole wafiwa pamoja na kujumuika nao kwenye wakati huu wa majonzi kwa ndugu, jamaa na marafiki wa familia.
Baadhi ya viongozi hao ni pamoja na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida ambaye baada ya kuhojiwa na mwanabari wetu alisema haya;
“Kusema kweli nimezipokea kwa masikitiko makubwa taarifa za msiba wa ndugu yetu Samuel Sitta, kwani marehem alimfahamu kwa utendaji wake mahili wa kazi wakati akiwa Spika wa Bunge letu huku akajulikana kwa jina la ‘Mzee wa Kasi na Viwango’.
“Alikuwa anajituma sana kufanya kazi zake tena kwa weredi na maarifa makubwa, tumempoteza mtu muhimu sana kwenye siasa za nchi na taifa kwa ujumla.”
Alipotakiwa kuzungumza kuhusu ratiba za maziko, Madabida alisema wasemaji wakuu ni ofisi ya bunge na serikali.
PICHA NA DENIS MTIMA/GPL
No comments:
Post a Comment