Advertisements

Monday, November 7, 2016

YANAYOENDELEA KUJIRI NYUMBANI KWA MAREHEMU SAMUEL SITTA Mwenyekiti  wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida akisaini kitabu cha maombolezo, wakati alipofika nyumbani kwa Marehemu Mh. Samuel Sitta aliekuwa Spika wa Bunge na Waziri Mwandamizi katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, aliefariki leo Novemba 7, 2016 huko nchini Ujerumani. Msiba upo Nyumbani kwa Marehemu, Masaki jijini Dar es salaam.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda (wa pili kulia) akiwa katika mazungumzo na baadhi ya viongozi pamoja ndugu wa Marehemu Mh. Samuel Sitta aliekuwa Spika wa Bunge na Waziri Mwandamizi katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, aliefariki leo Novemba 7, 2016 huko nchini Ujerumani.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kinondoni, Salum Madenge akisaini kitabu cha Maombolezo cha aliekuwa Spika wa Bunge na Waziri Mwandamizi katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, aliefariki leo Novemba 7, 2016 huko nchini Ujerumani.
Sehemu ya ndugu wa Marehemu wakiwa nyumbani hapo.

No comments: