ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, November 23, 2016

WAREMBO WA MISS UNIVERSE TANZANIA 2016 WAANZA KAMBI

NA ELISA SHUNDA,DAR

Warembo wa Miss Universe Tanzania 2016 wameanza rasmi kambi katika hoteli ya Colessium hii ni kwa ajili ya kujiandaa na fainali za mashindano hayo yanayotarajiwa kufanyika Novemba 25 jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa hoteli hiyo iliyopo Oysterbay.

Miss Universe Tanzania pia imeandaa mafunzo mbalimbali kwa ajili ya kuwapa warembo ili kujitambua kama vijana na kama wanawake hususani katika ujasiriamali, urembo na haiba . Mafunzo hayo yatakuwa yakitolewa na wataalamu mbalimbali toka katika Nyanja tofauti.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa jana,Mkurugenzi wa kampuni ya Compass Communications ambaye pia ndio Mkurugenzi na muandaaji mkuu wa kitaifa wa mashindano haya Maria Sarungi Tsehai alisema kuwa shindano la mwaka huu litakuwa zuri na la kipekee.


“Shindano la mwaka huu la Miss Universe Tanzania 2016 tumefanya usaili ambao ni mzuri sana lakini pia katika mfumo tofauti ukilinganisha na ilivyozoeleka warembo wetu wameonyesha vigezo vyote walivyoagizwa watume ambapo pamoja na kutuma video zao wakijibu maswali waliyotumiwa na kisha kuchujwa kwa kufuata mfumo huo lakini pia mkumbuke kuwa shindano hili la Miss Universe Tanzania tangu kuanzishwa kwake limefanikiwa kuifikia mikoa sita ikiwemo Dar es salaam, Dodoma, Arusha,Mwanza,Iringa na Mbeya” Alisema Sarungi

Kambi ya Miss Universe Tanzania 2016 imekamilishwa na warembo 10 ambapo waliofanikiwa kupata uwakilishi ni kutoka mkoa wa Dar es Salaam, Arusha, Dodoma na Mbeya.

Aidha mashindano hayo yalianza rasmi mwaka 2007 ambapo mrembo wake wa kwanza alikuwa ni Flaviana Matata ambaye mbali na kuliletea sifa Taifa pia amepata mafanikio makubwa katika fani ya ulimbwende kwa kuwa mwanamitindo wa kimataifa,wengineo waliofanikiwa kuchukua taji la Miss Universe Tanzania ni Amanda Ole Sulul 2008,Illuminata James 2009,Hellen Dausen 2010,Nelly Kamwelu 2011,Winfrida Dominique 2012,Betty Boniface 2013,Caroline Benaed 2014 na Lorraine Marriot mwaka 2015 ambaye ndiye atakayekabidhi taji kwa mshindi wa mwaka huu.

Mashindano ya Miss Universe Tanzania yamedhaminiwa na Best Western Plus Collesium Hotel, Compas Communications, Kwanza Tv na New York Film Academy.

Mwishoooooo                                         

No comments: