ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, December 25, 2016

Kwa waimbaji wa nyimbo za Injili Washington DMV!!

Je! Wewe ni mwimbaji wa muziki wa injili ama mpigaji wa ala za muziki?
Je! Ungependa kuwa mwimbaji wa muziki wa Injili ama mpigaji wa ala katika kumuimbia Mungu?
Kikundi cha nyimbo za injili cha Sounds Of Glory Singers kilichopo Washington DC kinaandikisha wanakikundi wapya kwa ajili ya huduma mpya na bora kuanzia Januari 2017.
Kama ni muimbaji, mpiga gitaa, drums, conga ama kinanda, unakaribishwa kujiunga na kikundi hiki.
Mazoezi ya kikundi hiki ni kila Jumamosi kuanzia saa kumi kamili jioni mpaka moja kamili usiku.
Kikundi kimedhamiria kuongeza vifaa vingi kuwezesha matamasha ya moja kwa moja jukwaani kuanzia Januari 2017.
Mwisho wa kujiandikisha ni Desemba 31, 2016
Kwa mawasiliano zaidi wasiliana na
Geofrey Kinyashi: 443 636 1781
Samuel Malonja: 240 752 5719
Mubelwa Bandio: 240 281 0574

KARIBUNI


No comments: