Advertisements

Sunday, December 11, 2016

NAPE: WADAU JITOKEZENI KUDHAMINI TUZO ZA MUZIKI NA FILAMU NCHINI.

Na Raymond Mushumbusi WHUSM.

Wadau wa Sanaa nchini wameshauriwa kujitokeza kudhamini tuzo kwa ajili ya wasanii wa muziki na filamu nchini ili kuendelea kuzipa nguvu tasnia hizo kwa maendeleo yake.

Ushauri huo umetolea jana na wazori wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye alipokuwa akizungumza katika hafla ya utoaji tuzo kwa wasanii wa muziki na Filamu nchini zilizoandaliwa na kituo cha Televisheni cha East Africa (Channel 5).

Ameongeza kuwa wadhamini wengi wajitokeze kwa ili kuongeza idadi ya tuzo zenye kiwango kinachostahili zenye kuzingatia weledi na usawa katika utoaji wake.“Niwaombe wadau wa sanaa nchini jitokezeeni kudhamini tuzo hizi za filamu na Muziki ili tuwe na tuzo nyingi zaidi na zenye viwango vya kimataifa”Alisistiza Mhe. Nnauye.


Kwa upande wake katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bw. Godfrey Muingereza amesema kuwa BASATA itaendelea kushirikiana na wasanii na wadau wa Sanaa katika kuandaa na kusimamia tuzo mbalimbali ikiwa ni nia ya Serikali kuikuza tasnia ya muziki na filamu ambayo ni moja ya tasnia inayoajiri vijana wengi kwa sasa.

“Nawaalika wadau wa Sanaa na wasanii wote sisi tuko tayari kushirikiana nao katika kulisukuma hili guruduma la maendeleo ya Sanaa nchini na nawasahuri tufate tu utaratibu katiaka kuandaa kazi zenu za sanaa” alisema Bw. Muingereza.

Aidha mwakilishi wa Bodi ya Filamu Tanzania Bw.Romanus Tairo amesisitiza wasanii wa filamu nchini kufata sheria na gtaratibu zote kabla ya kuandaa na kusambaza filamu zao.

“Nawaomba wasanii wote wa filamu nchini kufuata Sheria na taratibu zilizopo za kusajili filamu zote zikakaguliwa na kuoewa kibali cha kuoneshwa sehemu mbalimbali”Alisema Bw.Tairo.

No comments: