Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Lilian Liundi akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina iliyowakutanisha wadau wa kutetea haki za mwanamke ili kujadili juu ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDG s) hasa kwenye lengo namba tano linalohusu usawa wa kujinsia.
Balozi Gertrude Mongella akizungumza wakati alipokuwa anafungua mkutano wa wadau mbalimbali wa kutetea haki za mwanamke ili kujadili malengo ya Maendeleo Endelevu (SDG s) hasa lengo namba tano ulioandaliwa na TGNP Mtandao leo katika ukumbi wa Hotel ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam leo.
Mwanachama na mwanzilishi wa Shirika lisilo la kiserikali la TGNP Mtandao, Bi. Zipora Shekilango akitoa historia yake na mchango wake katika shirika la TGNP Mtandao leo katika mkutano uliowakutanisha wadau mbalimbali wa kutetea haki za mwanamke uliofanyika katika ukumbi wa Hotel ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam leo.
Mkuu wa Program ya Taarifa na Utafiti kutoka TGNP, Gloria Shechambo akitolea ufafanuzi kwa baadi ya mambo wakati wa mkutano huo.
Baadhi ya wadau mbalimbali kutoka serikalini na sekta binafsi wakifuatilia mada za kwenye mkutano uliowakutanisha kujadili kujadili malengo ya Maendeleo Endelevu (SDG s) hasa lengo namba tano ulioandaliwa na TGNP Mtandao leo katika ukumbi wa Hotel ya Protea.
Picha ya Pamoja
No comments:
Post a Comment