Advertisements

Wednesday, January 25, 2017

Ajali ya Basi na Lori la Mbao Yaua na Kujeruhi 32 Iringa

Mtu mmoja amefariki dunia na wengine 32 kujeruhiwa vibaya baada ya basi la Vitu Laini linalofanya safari zake kutoka vijiji vya Kilolo kwenda Iringa Mjini kugongana na lori la mbao karibu likiwa limekaribia kufika Iringa Mjini.
Akizungumza na Global Publishers, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, ACP Peter Kakamba amethibitisha kutokea kwa ajli hiyo na kueleza kuwa majeruhi wote wa ajali hiyo wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Iringa.
\
“Ni kweli ajali imetokea leo asubuhi nje kigogo ya Mji wa Iringa, basi ndilo limelogonga lori kwa nyuma na kusababisha kifo cha mtu mmoja aliyeaga dunia palepale na kusababisha majeruhi 32.

“Majeruhi wote tumewapeleka katika Hospitali ya Mkoa wa Iringa ambako wanaendelea kupatiwa matibabu mpaka sasa. Alisema Kamanda Kakamba.
Kuhusu chanzo cha ajali hiyo haijafahamika kama ni matatizo ya gari au mwendoksasi wa dereva hivyo Kamanda Kakamba amesema watatoa taarifa rasmi baabdaye kuhusu tukio hilo. GPL

No comments: