ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, January 29, 2017

ALIKIBA YAZINGATIE MALALAMIKO YA MASHABIKI WAKO


Ali Saleh Kiba al maarufu kama Alikiba ni miongoni mwa wasanii wakongwe na wakubwa Tanzania, Afrika Mashariki na pengine Afrika kwa ujumla. Ni mshindi wa tuzo zaidi ya 14 kwa mwaka 2016 ikiwezo tunzo kubwa kabisa za MTV EMA kwa kipengele cha Best African Act.


Kwa mafanikio makubwa aliyoyapata mwaka jana ikiwemo kupata mkataba mnono wa kampuni kubwa ya muziki duniani yaani Sony Music na kushinda tuzo zote hizo ndani ya mwaka 2016 ni wazi kabisa kuwa thamani ya Alikiba imepanda maradufu barani Afrika na pengine kila mfuatiliaji wa muziki Afrika angependa zaidi kumfahamu Alikiba, kufahamu kazi zake, ni wapi ametoka na wapi anakwenda.
Sekeseke lilitokea mwaka jana kwenye show ya Mombasa rocks iliyofanyika mjini Mombasa, Kenya kati ya Wizkid na Alikiba ni moja kati ya mambo ambayo yalifanya jina la Alikiba lizungumzwe sana barani Afrika haswa Tanzania, Kenya na Nigeria ambapo mitandao mbalimbali ya Nigeria iliripoti kua Alikiba anatrend sana nchini Nigeria.

Ushindi wa MTV EMA pia ambao awali alipewa Wizkid kabla haujatenguliwa na kupewa Alikiba ni mambo yaliyofanya apate attention zaidi kwenye soko la muziki barani Afrika.

Kutrend ni kitu muhimu sana katika soko la muziki kwa sasa, wasanii wengi duniani kote hata mpaka Marekani wamekuwa wakitengeneza kiki kabla ya kuachia kazi zao mpya ili kupata attention. Nafahamu kuwa msanii Alikiba amekuwa sio muumini mzuri sana wa kiki, lakini kiki kama hizi ambazo zinajitengeneza zenyewe ni dhambi kubwa kuacha kuzitumia kibiashara sababu kuna wanaotamani kutrend hata kwa kutembea uchi lakini hawazipati.

Mapema mwaka huu Alikiba alitangaza ratiba ya World Tour yake itakayoanzia South Africa kisha America na kumalizikia barani Ulaya. Kwa mujibu wa ratiba kutoka kwenye posters zake alizozipost Instagram Tour yake inaanza February mwaka huu. Hivyo mpaka ninaandika makala hii zimebaki siku tatu kufikia mwezi February.

Kati ya sehemu ngumu sana kupenya kimuziki barani basi ni Afrika Kusini na hii imetokana na ‘wasauzi’ kuthamini sana muziki wao na haikushangaza licha ya jina kubwa alilojijengea Diamond Platnumz kwenye kiwanda cha muziki barani Africa aliwahi kaririwa akisema amefanya collaboration na AKA ili kupenyeza muziki wake África Kusini.

Sasa wasiwasi wangu ni je? Alikiba anategemea kujaza viti kwa kuitegemea nyimbo ya Aje pekee? Target yake kwenye hii tour ni kuifanya iwe ya kidunia au analenga waTanzania pekee wanaoishi kwenye nchi husika? Aliahidi atatoa Aje remix ambayo ni nyimbo aliyoimba na msanii kutoka Nigeria MI Abaga lakini mpaka zimebaki siku tatu kabla hatujaingia mwezi anaoanza tour hakuna dalili ya hiyo nyimbo?

Binafsi nilidhani ingekuWa sahihi sana kama angeachia nyimbo ambayo amesharekodi mama mkongwe Yvonne Chakachaka kwa lengo la kuiteka zaidi South Africa kibiashara zaidi ili jina lake liwe kubwa nchini humo hata wakati wa Tour yake angetumia pia na fursa hiyo kufanya media tour kuitambulisha zaidi hiyo ngoma.

Nadhani si Mimi ila asilimia 98 ya mashabiki hawaridhishwi na namna ambayo Alikiba amekuwa slow sana na kutojua namna soko la mUziki linavyoenda na nini linataka. Ni jana kupitia mtandao wa instagram msanii wa maigizo ambaye pia ni shabiki mkubwa wa msanii Alikiba alipost kipande cha screenshot kikionesha ujumbe aliotumiwa na shabiki mwingine wa Alikiba DM kua Ali atapoteza mashabiki wake sababu hawapi raha wanayoitaka, siku zote amekuwa mtu wa kujiamini na kuwasibirisha mashabiki wake ambao ukweli bila wao asingekua hapo halipo leo.

Mwaka mpya umeanza kwa kasi kweli kila mtu yuko kasi lakini naona Alikiba bado yule yule.

Imeandikwa na Javan Watson
Instagram: @JavanOfficiel
twitter: @JavanWatson

No comments: