Mtuhumiwa huyo baada ya kuua mzazi wake alimfungia ndani ya stoo ya nyumba aliyokuwa akihifadhi vyuma chakavu.
Diwani wa Mbogi ambaye pia ni Mwenyekiti wa kijiji cha Kebeyo, Ezekel Kebaki na kaka wa marehemu, Werema Chacha, wameeleza hayo kwa nyakati tofauti.
Kebaki amesema tukio hilo lilitokea kijijini Kebeyo jana usiku nyumbani kwa Nyakogera (marehemu) wakati alipokuwa akiingia katika stoo, kukagua vyuma chakavu katika stoo yake anayotunzia vifaa hivyo.
Kebaki alisema Marwa (mtuhumiwa), alikuwa katika stoo hiyo akiwa amepitia kwenye tundu alilotoboa na kukumbana na baba yake huyo mzazi na kuanza kumshambulia kwa nondo kichwani na kufa papo hapo.
Alisema baada ya kitendo hicho, mtuhumiwa alifunga mlango kwa nje na kutoroka.
Kaka wa marehemu, Chacha alisema iligundulika kuwa Nyakogera (marehemu) amekufa baada ya watu kwenda kumuangalia baada ya kutotoka katika stoo hiyo kwa muda mrefu.
Chacha alisema kulikuwa na mgogoro kati ya mdogo wake (marehemu) na mtoto wake.
Inadaiwa kuwa, Novemba mwaka jana kijana huyo alimwibia baba yake Sh 900,000 za mauzo ya asali kutoka mizinga 200 aliyonayo.
Alisema baba yake alimkamata na kumfungulia kesi ambayo ipo mahakamani na kijana huyo alidhaminiwa hivyo alikuwa nje kwa dhamana.
"Kumekuwa na vitisho kwa mzazi wake huyo na kwa sasa baada ya tukio hili la mauaji ya baba, kijana huyo haonekani na anatafutwa kwani alikuwepo kabla ya mauaji, lakini sasa hivi ametoroka haonekani, tunasaidiana na wananchi na Polisi kumsaka" amesema Chacha.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Tarime/Rorya, Andrew Satta alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Alisema Polisi inamsaka mtuhumiwa.
Aliwaomba wananchi washirikiane na Polisi kuhakikisha anatiwa mbaroni.
HABARI LEO
No comments:
Post a Comment