Wamekamatwa kwa tuhuma za kufuja michango ya wananchi, iliyokusanywa kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo.
Wengine waliokamatwa pamoja naye ni Ramadhan Hangahane (45) na Swadikina Maulid (41), wote wakazi wa vijiji vya Ihowanja na Kilosa Kwa Mpepo.
Watuhumiwa hao walikamatwa kwa amri ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk Kebwe Stephen Kebwe, jana wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Kilosa Kwa Mpepo, baada ya wananchi kuibua hoja ya kata hiyo kutokuwa na shule ya sekondari.
Mkazi wa kata hiyo, Juliana Moris, katika hoja yake kwa Mkuu wa Mkoa , amesema, uongozi wa kata hiyo chini ya Lijola na kamati ya ujenzi wa shule hiyo, ilikusanya michango ya wananchi kila mmoja Sh 17,500 , lakini hakuna kilichofanyika na fedha hazijulikani zilipo. Juliana alisema kata hiyo hadi sasa haina sekondari na watoto wao waliofaulu kuendelea na masomo ya sekondari, wanalazimika kuwagharimia kuwapangishia makazi katika kata ya Ngoheranga, umbali mrefu kutoka Kilosa Kwa Mpepo.
Kufuatia hoja na mkazi huyo, ambayo uliungwa mkono na wananchi wa waliokuwa katika mkutano huo kutoka vijiji viwili vinavyounda kata hiyo kuwa fedha walizochanga zimeliwa na kamati ya ujenzi, ambapo walidai ni zaidi ya Sh milioni tatu.
Kitendo hicho kilimlazimu, mkuu wa mkoa kumwagiza mkuu wa Polisi wa wilaya hiyo kuwatamata wajumbe kamati ya ujenzi waliotajwa pamoja na Kaimu Ofisa Tarafa ya Ngoheranga, ambapo awali alikuwa ni Mtendaji wa kata ya Kilosa Kwa Mpepo kabla ya kuhamishiwa kata ya Biro na kukaimu nafasi ya Ofisa Tarafa.
Pia Dk Kebwe alivunja kamati ya ujenzi wa shule, ambayo ilikuwa ikihusiana na uchangishaji wa michango ya wananchi kwa ajili ya ujenzi huo.
Kebwe alimwagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi, Marcelin Ndimbwa, kutuma wakaguzi wa ndani kwa ajili ya kuchunguza upotevu wa michango ya wananchi. Alisema ikithibitika viongozi wa Serikali za vijiji hivyo, wamekula fedha hizo wafunguliwe mashitaka mahakamani na kuvuliwa nafasi zao.
HABARI LEO
No comments:
Post a Comment