ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, January 12, 2017

DKT. SHEIN AONGOZA SHEREHE ZA MAPINDUZI YA ZANZIBAR KATIKA UWANJA WA AMANI LEO

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein akiongea na wananchi wakati wa sherehe za miaka 53 ya mapinduzi ya Zanzibar ambapo alisema mbali za jitihada zilizofanywa na serikali hiyo katika kuinua maisha ya wazanzibar ameahidi kuendelea kusimamia rasilimali ili zitumike kwa maslahi ya wananchi wote.
Makamo wa Pili wa Rais Zaznzibar Balozi Seif Ali Idd akiongea na wananchi wakati wa sherehe za miaka 53 ya mapinduzi ya Zanzibar ambapo alisema serikali ya mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kuweka jitihada ili kuendelea kujenga uchumi za Zanzibar kwa maslahi ya wananchi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein akiwasalimia wananchi walijitokeza katika sherehe za miaka 53 ya mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Amani, Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein akiimba wimbo wa Taifa katika sherehe za miaka 53 ya mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Amani, Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein akikagua gwaride katika sherehe za miaka 53 ya mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Amani, Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein akisalimiana na viongozi wastaafu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika sherehe za miaka 53 ya mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Amani, Zanzibar.
Rais Mstaafu wa Zanzibar, Aman Karume akiteta na  Rais Mstaafu wa Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete katika maadhimisho ya miaka  53 ya Mapinduzi  ya Zanzibar  zilizofanyika kwenye uwanja wa Aman Zanzibar Januari 12, 2017.
 Baadhi ya waandamanaji wakishangilia  wakati walipopita mbele ya Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohammed  Shein katika maadhimisho ya  miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar kwenye uwanja wa Aman, Zanzibar Januari 12, 2017.




Vikundi mbalimbali, Asasi za Kiraia,Vyama vya Siasa,Mikoa,Wizara na Taasisi za Serikali wakipita mbele Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein katika sherehe za miaka 53 ya mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Amani, Zanzibar.

Vikosi mablimbali vya Jeshi la Polisi vikipita mbele Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein katika sherehe za miaka 53 ya mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Amani, Zanzibar.
Askari wa Kikosi cha Zimamoto na Uokozi cha Zanzibar akipita   kwa ukakamavu mbele ya  mgeni rasmi Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohammed Shein  katika gwaride la kuadhimisha miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar Januari 12, 2017 
Vijana vya halaiki wakiwa katika umbo linaloonesha miaka 53 ya mapinduzi ya Zanzibar katika sherehe zilizofanyika katika uwanja wa Amani, Zanzibar.

Kikosi cha Kwata la KimyaKimya wakionesha onesho wakati wa sherehe za miaka 53 ya mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Amani, Zanzibar.

Komando wa Jeshi la Wananchi Tanzania akishuka katika kamba katika sherehe za miaka 53 ya mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Amani, Zanzibar.
18-Kikosi cha Makomandoo wa Jeshi la Wananchi Tanzania wakionesha onesho wa namna ya kuakibiana na vikwazo mbalimbali wawapo kazini katika sherehe za miaka 53 ya mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Amani, Zanzibar.
Askari wa Kikosi cha Mbwa, akionesha namna mbwa anavyoweza kuruka vikwazo mbalimbali katika kukabiliana na wahalifu katika sherehe za miaka 53 ya mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Amani, Zanzibar.
 Mmoja wa wananchi wa Zanzibar akimsikiliza kwa makaini Rais wake, Dkt. Ali Mohammed Shein  wakati alipohutuba katika Maadhimisho ya  miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar  kwenye uwanja wa Aman Januari 17, 2017. 
  Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohammed Shein, Makamu wa Rais, Samia Suluhu, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Sif Idd wakifuatilia kwa makini gwaride  la Maaddhisho ya miaka 53  ya Mapinduzi ya Zanzibar kwenye uwanja wa Aman, Januari 12, 2017.
 Makomandoo wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania  wakionyesha uwezo wao wa kupigana bila silaha katika Maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar kwenye wawnja wa Aman Januari 12, 2017. 

No comments: