ANGALIA LIVE NEWS

Friday, January 20, 2017

DONALD TRUMP AWA RAIS WA 45 WA MAREKANI

Donald Trump ameapishwa kuwa rais wa 45 wa Marekani. Trump amechukua hatamu kutoka kwa Rais Barack Obama saa mbili usiku kwa muda wa Afrika Mashariki. Wafuasi wake walikusanyika kwa wingi barabara za Washington.
Donald Trump amekuwa rais wa 45 wa Marekani amerejelea ahadi yake ya kampeni ya kuifanya nchi yake kuwa taifa lenye nguvu zaidi kuliko hapo awali, Hata hivyo maelfu waandamana nchini Marekani kupinga kuapishwa kwake.

Rais wa 45 wa Marekani, Donald Trump pamoja na familia yake wakifurahia mara baada ya kumaliza kuapishwa kwa rais mpya wa Marekani.
Rais wa 45 wa Marekani, Donald Trump akihutubia taifa kwa mara ya kwanza mara baada ya kuapishwa kuwa rais wa Taifa hilo.

Baadhi ya wananchi waliokuwa wanashuhudia kuapishwa kwa Donald Trump
Rais wa 45 wa Marekani, Donald Trump(mwenye tai nyekundu) akimsindikiza rais aliyemaliza muda wake Barack Obama pamoja na aliyekuwa Makamu wa rais wake 
Rais wa Marekani, Donald Trump akipeana mkono na rais aliyemaliza muda wake Barack Obama 

 Rais aliyemaliza muda wake Barack Obama akiwapungia mkono 
Herikopta  iliyombeba rais aliyemaliza muda wake Barack Obama pamoja na mke wake ikiondoka 

No comments: