Mbunge Mteule wa Rais, Anne Kilango Malecela amesema uteuzi wake umetokana na uwezo alionao na si vinginevyo.
Akizungumza na Gazeti la Mtanzania kwa njia ya simu Jumapili hii, Kilango alisema anamshukuru Rais Magufuli kwa kutambua uwezo wake wa kuchapa kazi huku akiahidi kuendelea kuwatetea wananchi wa Same Mashariki na Watanzania kwa ujumla.
Alisema “Namshukuru sana Rais kwa kutambua uwezo wangu kwa kuwa nilishawahi kuwa mbunge nina uzoefu nitaendelea kupigania maendeleo ya wananchi na jimbo langu nitapambana kwa ajili ya nchi yangu pia.”Nina nyumba zangu na mashamba yangu huko Same hivyo nawaambia wananchi wa Same na wananchi wote kwa ujumla narudi bungeni kuwatetea”.
Aidha Kilango alisema atafanya kazi kwa moyo wote kuwakilisha Tanzania na chama chake bila ubaguzi. Kilango aliteuliwa juzi usiku na Rais Dk. Magufuli kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu iliyosainiwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa, mbunge huyo ataapishwa kwa mujibu wa taratibu za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
No comments:
Post a Comment