ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, January 19, 2017

Lipumba, Sumaye ‘wagongana’

Kutoka kushoto ni Profesa Ibrahim Lipumba na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Frederick Sumaye wamekutana kwenye kampeni za uchaguzi wa diwani wa Kata ya Kahumulo huku kila mmoja akirusha vijembe kwa chama cha mwenzake.

By Mwandishi Wetu, Mwananchi mwananchipapers@mwananchi.co.tz

Mikoani. Mwenyekiti wa CUF anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Frederick Sumaye wamekutana kwenye kampeni za uchaguzi wa diwani wa Kata ya Kahumulo huku kila mmoja akirusha vijembe kwa chama cha mwenzake.

Wakati Lipumba akiielezea Chadema kuwa imepoteza mwelekeo kwa kumkaribisha waziri huyo mkuu wa zamani na mwenzake, Edward Lowassa, Sumaye amesema CUF haiwezi kuwakomboa wakazi wa Kahumulo.

Wawili hao walikuwa katika kata moja wakiwanadi wagombea udiwani wa vyama vyao katika mikutano miwili tofauti ya uchaguzi mdogo uliopangwa kufanyika Jumapili ijayo.

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wa kumnadi Ntalikwa Ishatala uliofanyika Kata ya Kahumulo, Profesa Lipumba amesema Chadema ni chama kilichopoteza mwelekeo kwa kuwa kimebeba mafisadi waliohama CCM.

Wakati Profesa Lipumba akiishambulia Chadema, Sumaye alikuwa eneo jingine akimnadi mgombea wa chama hicho kwenye kata hiyo, Dotto John.

Waziri huyo mkuu wa Serikali ya Awamu ya Tatu amesema CUF na CCM ni vyama ambavyo havina mtazamo wa kuikomboa Tanzania.

No comments: