Tanga. Wanafunzi wa Chuo cha Uguuzi na Ukunga kilichopo Bombo mkoani Tanga wamegoma kushiriki masomo wakishinikiza kurejeshewa huduma ya maji na umeme kwenye mabweni yao.
Baadhi ya wanafunzi hao wamesema kuwa wamekosa huduma hizo kwa kipindi kirefu na hakuna hatua zozote zilizochukuliwa licha ya kufikisha malalamiko yao kwenye uongozi wa chuo.
Mmoja wa wanafunzi wa mwaka watatu katika chuo hicho, Emmanuel Amoni amesema wametoa kilio hicho kwa uongozi lakini cha kushangaa tatizo hilo wameliona kama la kawaida wakati wanaumia.
No comments:
Post a Comment