Rais wa Marekani Donald Trump
amechukua hatua ya kwanza akiwa madarakani, kutia saini agizo lake la
kutaka kufanyiwa mabadiliko ya sera ya matibabu ya rais aliyemaliza
muda wake Barack Obama.
Agizo hilo la rais Trump,
limeziagiza taasisi husika kuangalia namna ya kupunguza mzigo wa
kiuchumi uliosababishwa na sheria ya matibabu, inayojulikana zaidi
nchini humo kama Obamacare.
Akiapishwa jana rais Trump, aliahidi
kuanzia jana kuwa ataweka maslahi ya Marekani kwanza, kufufua viwanda
na kujenga miundombinu ya Marekani ambayo amesema imeoza na
kutelekezwa.
Baadaye leo kundi la wanawake
200,000 wameahidi kushiriki maandamano ya Wanawake Jijini Washington,
ambayo waandaji wamesema yanalenga kuangazia ubaguzi na suala la
usawa ambalo linakabiliwa na tishio chini ya utawala wa Trump.
No comments:
Post a Comment