HII kali! Baada ya kuolewa na ndoa kudumu kwa siku saba tu, msanii wa Bongo Fleva na filamu, Sabrina Omary ‘Sabby Angel’ ameweka wazi kuwa anajuta kuolewa na Mwarabu.
Sabby ambaye aliolewa na Mwarabu aliyefahamika kwa jina la Jaruf alisema, hatothubutu tena kuolewa na watu wenye asili hiyo kwani amebaini hatawezana nao kutokana na tabia zao.
“Mimi tena? Hapana, sitathubutu kuolewa tena na Mwarabu. Nimekuwa katika mahusiano tofauti na wanaume wa Kiafrika lakini sijaona kimbembe kama nilivyokuwa na yule Mwarabu, sitarudia kosa,” alisema Sabby anayetikisa na Wimbo wa Inahusu.
GPL
No comments:
Post a Comment