Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kupata pigo baada ya wanachama 200, wakiwamo viongozi wa Kitongoji cha Kwemghogho Mahezangulu kujitoa na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) .
Akizungumza baaada ya kupokea wanachama hao, Mbunge wa Bumbuli, January Makamba (CCM), alisema wananchama hao wameamua kurudi wenyewe nyumbani kutokana na kuona ahadi nyingi za maendeleo zimetekelezwa kwa kiasi kikubwa.
Alisema chama chake kimefanya mambo mengi hivyo haoni ajabu ya kupokea wanachama kutoka vyama vingine vya upinzani.
January, ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira, alisema hivi sasa kuna kazi kubwa ya kuendelea kuleta maendeleo ambayo yanahitaji umoja na mshikamano.
Alisema migogoro, majungu na fitina inatokana na kambi zilizokuwapo huku akiwasisitiza wana CCM watambue ni hema kubwa na linavumilia tofauti za watu.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Kitongoji cha Kwemghogho, Shabani Kahema, aliwataka vijana na wanachama wengine kubadilika kwa kuwa CCM ndiyo chama chenye ilani inayotekelezeka.
No comments:
Post a Comment