ANGALIA LIVE NEWS

Friday, January 20, 2017

WAZIRI UMMY AAGIZA WAKUNGA NA WAUGUZI WASIKAMATWE BILA YA KUFUATA TARATIBU ZILIZOPO.

 Waziri wa Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiongea na wadau wa Baraza la Baraza la Wakunga hawapo pichani wakati wa kuzindua mradi wa Mkunga Okoa Maisha kwa kushirikiana na watu wa Canada.
Waziri wa Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu katikati akikata utepe kuashiria kuzindua  mradi wa Mkunga Okoa Maisha , wa kwanza kushoto ni Balozi wa Canada  Bi. Susan Steffan na wakawnza kulia ni Katibu Mkuu wa Baraza la Wakunga nchini Dkt. Sebalda Leshabari.


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ametoa agizo kwa viongozi wote nchini kuacha mara moja kuwakamata wauguzi,  wakunga na kuwaweka ndani na badala yake wanapaswa kufuata taratibu zilizopo.
Akizungumza  hayo wakati wa uzinduzi wa mradi wa Mkunga Okoa Maisha Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto  Ummy Mwalimu  alisema wakunga wanalo baraza ambako ndilo suluhishi la matatizo yao.
"Aidha Mhe. Ummy amesema kuwa pale ambapo muuguzi au mkunga anapokosea  zipo taratibu za kufuata na siyo kumweka ndani kwani kuna Baraza la Wakunga ambalo lina Mamlaka ya kisheria za kuchukua kwa mkunga yoyote ambaye amekwenda kinyume.
"Tunao Wakunga na wauguzi ambao wanafanya kazi zaidi ya masaa, tumeona kilichotokea Sikonge, kiongozi anakuja juu kwanini mtoto amepewa dawa ya Quinn," alisema Ummy.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Baraza la Wakunga nchini Dkt. Sebalda Leshabari amesema kuwa mradi huo unalenga  kupunguza vifo katika Mikoa ya Shinyanga na Simiyu hivyo wauguzi na wakunga ni vema wakashirikiana na Baraza hilo ili kufanikisha malengo yao.

No comments: