Timu ya Azania Group, ndiyo itakayowakilisha Tanzania katika mashindano ya kikanda ya Afrika Mashariki, ya Benki ya “Standard Chartered-Road to Anfield” yatakaofanyika uwanja wa Jakaya Kikwete Youth Park Jumamosi, Machi 4. Azania walipata ushindi huo kwa kuichakaza timu ya H&R Consultancy mabao ya 6-5 kwa penati dhidi ya katika mchezo wa kukata na shoka uliofanyika mwishoni mwa wiki na kufanikiwa kuipeperusha bendera ya Tanzania. Kwa maana hiyo, Azania Group wanatarajia kumenyana uso kwa uso na washindi wa michuano hiyo kutoka nchi za Kenya na Uganda. Washindi wa michuano hiyo nchini Uganda ni timu ya Cocacola wakati kidedea wa kombe hilo nchini Kenya ni Radio ya Capital FM.
Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered, Tanzania Sanjay Rughani (kushoto) na Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki hiyo, Juanita Mramba wakikabidhi kikombe kwa Bw Sikaba Hamisi ambaye ni Nahodha wa timu Azania Group, Mshindi wa kitaifa wa mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017 (Road to Anfield), mashindano yaliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye viwanja vya JK Youth Park, Gerezani jijini Dar es Salaam.
Akiongea na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kutwaa ushindi huo, Nahodha wa Azania Group, Bw. Shabaka Hamisi alisema maandalizi yao mazuri ndiyo siri ya ushindi wao na kuongeza kwamba wapo tayari kuwanyoa hao wageni asubuhi kabisa. “Katika jambo lolote kama unataka kufanya vyema, maandalizi mazuri yanasaidia sana. Kwa upande wetu, tulifanya mazoezi yakutosha na ndiyo maana leo tumeibuka washindi.” Alisema. Aliongeza, “Siyo kwamba wenzetu walikua wabovu, ila umakini na utulivu kwa upande wa wachezaji wangu ndiyo kilichotusababishia kupata matokeo mazuri.”
Alisema mazoezi ya kujipanga kwa ajili ya mechi tayari yameshaanza kwa ari na nguvu mpya, akiongeza kuwa ushindi kwao ni lazima. Kwa upande wake, Phillip David, nahodha wa H&R Consultancy alisema kukosekana kwa ukosefu wa umakini katika ushambuliaji ndiyo uliosababisha timu yake kupoteza mechi hiyo, hata hivyo alishukuru kwa kuibuka mshindi wa pili wa mashindano hayo.
Alisema mazoezi ya kujipanga kwa ajili ya mechi tayari yameshaanza kwa ari na nguvu mpya, akiongeza kuwa ushindi kwao ni lazima. Kwa upande wake, Phillip David, nahodha wa H&R Consultancy alisema kukosekana kwa ukosefu wa umakini katika ushambuliaji ndiyo uliosababisha timu yake kupoteza mechi hiyo, hata hivyo alishukuru kwa kuibuka mshindi wa pili wa mashindano hayo.
Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered, Tanzania Sanjay Rughani (kushoto) na Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki hiyo, Juanita Mramba (kulia) wakifurahi katika picha ya pamoja na timu ya Azania Group wakikabidhi kikombe kwa timu Azania Group,Mshindi wa kitaifa wa mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017(Road to Anfield), mashindano yaliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye viwanja vya JK Youth Park,Gerezani jijini Dar es Salaam.
“Kama ulivyoona, mechi ilikuwa moja moja hadi tukaingia kwenye matuta. Wenzetu walipata penati sita wakati sisi tulifunga tano. Nafasi ya kushinda ilikuwa upande wetu lakini Mungu hakupenda iwe ivyo,” alisema. Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered Tanzania Limited, Sanjay Rughani aliwaasa wachezaji wa Azania Group kuwa wajiandae kikamilifu ili waubakishe ubingwa nchini Tanzania. “Sisi hakuna zawadi nzuri ambayo tunaitaka kutoka kwenu zaidi ushindi. Fanyeni mazoezi ya kutosha ili Jumamosi inayokuja muweze kushinda mechi zenu zote dhidi ya hizo timu kutoka Kenya na Uganda. Na sisi kama wadhamini tutakua pamoja nanyi ili kuhakikisha kwamba mnapata ushindi hapa nyumbani,” alisema Sanjay. Naye Mkuu wa Masoko na Uhusiano wa Benki hiyo, Juanita Mramba, aliwapongeza kwa ushindi huo lakini akiwatahadharisha kuwa safari yao ndiyo kwanza imeanza. “Leo mmeshinda mashindano haya, Jumamosi kazi yenu ni kubwa zaidi kwani mtacheza na wageni wawili, hivyo jipangeni vizuri zaidi mkiutumia vyema uwanja wa nyumbani,” alisema. Ukiachia mbali Azania ambao waliondoka na kombe za dhahabu, washindi wa pili H&R Consultancy walijitwalia kombe la shaba, huku washindi wa tatu PWC wakitwaa kombe la Bronze.
Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered, Tanzania Sanjay Rughani (kushoto) akikabidhi kombe kwa Nahodha wa timu ya HR Consultants, Phillip David ambao ni washindi wa pili wa mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017 (Road to Anfield), yaliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye viwanja vya JK Youth Park, Gerezani jijini Dar es Salaam. Anayeshuhudia tukio hilo ni Mkuu wa Wateja Binafsi wa Benki ya Standard Chartered, Michael Shio (kulia).
No comments:
Post a Comment