Mkurugenzi wa halmashauri ya Ileje Haji Mnasi akiwa kwenye harambee ya uchangiaji wa vifaa vya ujenzi wa zahanati ya ushirika wa Rungwa iliyopo katika wilaya ya Ileje.
Na Fredy Mgunda.
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Ileje Haji Mnasi afanikisha azima ya ujenzi wa zahanati bora katika ushirika wa Rungwa kwa lengo la kuboresha huduma za afya kwa wananchi wa wilaya ya Ileje.
Akizungumuza wakati wa
harambee ya kuchangia ujenzi wa zahanati hiyo mkurugenzi Mnasi alisema kuwa wameamua
kuendelea kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea
kuboresha hutuma za afya kwa wananchi ili wafanye kazi kwa kujituma.
“Kauli mbiu ya Rais wetu ni
hapa kazi tu sasa ukiwa na jamii ambayo dhohofu huwezi kufikia malengo ya hapa
kazi hivyo nimefanya harambee hii kumuunga mkono Rais kwa kuboresha huduma za
afya katika wilaya yetu ya Ileje na kuwafanya wananchi kufanya kazi kwa
kujituma huku wakiwa na afya njema na kuendelea kulijenga taifa kwa kufanya
kazi kwa kujituma”.alisema Mnasi
Mnasi alisema wananchi
wanatakiwa kujitoalea kwa hali na mali kufanikisha ujenzi wa zahati hiyo unakamilika
kwa wakati na kuanza kutoa huduma kwa jamii.
“Leo hii tumefanya harambee
ya kuchangia kupatikana kwa vifaa vya kumalizia ujenzi wa zahanati unaogharimu
kiasi cha shilingi milioni sita na nashukuru mungu nimefanikiwa zaidi kupata shilingi
milionii nne hivyo lengo limetimia kilicho baki ni utekelezaji tu
labda niwaombe kuzitumia pesa hizi vizuri kununua vifaa ya ujenzi ili wananchi
waanze kupata huduma bora”. Alisema Mnasi
Aidha Mnasi alizitaka taasisi
nyingine kuiga mfano wa ushirika wa Rungwa kwa ujenzi wa zahanati hiyo ambayo
itarahisisha uwepo wa huduma bora kwa jamii husika.
“Tuna taasisi nyingi sana
katika wilaya yetu hivyo naziomba nazo zijitahidi kuwa na malengo ya ujenzi wa
zahanati ili kuendeleza kutoa huduma bora kwa jamii na kuifanya jamii kuwa huru
kufanya kazi kwa nguvu huku wakiwa na afya bora”.alisema Mnasi
Nao baadhi ya waumini wa
ushirika wa Rungwa walimushukuru Mkurugenzi huyo kwa kuendelea kujituma kufanya
kazi kwa wananchi wa chini na kuwaboresha huduma za afya.
“Tulikuwa tunahitaji zaidi
ya milioni sita lakini uwepo wa mkurugenzi Mnasi katika harambee ya leo
kumesaidia kupata pesa nyingi ambazo zimefanisha azma ya umaliziaji wa ujenzi
wa zahanati yetu”.walisema washirika
No comments:
Post a Comment