ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, February 26, 2017

CHIMELEDYA: WAUMINI MSICHANGANYWE NA MANENO

Askofu Mkuu wa Anglikana Tanzania, Dk Jacob Chimeledya amesisitiza kuwa dayosisi ya Dar es Salaam ipo chini yake katika kipindi hiki baada ya Askofu Dk Valentino Mokiwa kuamriwa kujiuzulu.
Aliwataka waumini wasichanganywe na maneno kwani taratibu na katiba ilifuatwa katika kumuondoa Mokiwa.
"Nawaomba waumini wa kanisa hili kuwa watulivu, msichanganye na maneno yanayosemwa juu ya uamuzi wa kumtaka Dk Mokiwa kujiuzulu.Tulifuata taratibu zote na hivi sasa mimi ndiye msimamizi mkuu wa dayosisi hadi hapo askofu wa jimbo atakapopatikana," amesema Dk Chimeledya
Dk Chimeledya ametoa msisitizo huo leo wakati aliposhiriki ibada ya misa ya asubuhi iliyoongozwa na Jaji mstaafu Augustino Ramadhan iliyofanyika katika kanisa la St Albano Posta na kusema kuwa Katiba inaruhusu yeye kulisimamia kanisa kutokana na Mokiwa, kutakiwa kujiuzulu .
Amesema mchakato wa kumuamuru Dk Mokiwa aliyekuwa askofu mkuu wa dayosisi hiyo ulifuata sheria , kanuni na katiba ya Anglikana iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2004.

No comments: