Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Fortunatus Kapinga, akizungumza wakati akimkaribisha Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika hilo, Dk. Haruni Kondo (katikati), kuzungumza na waandishi wa habari, Makao Makuu ya shirika, Dar es Salaam jana. Kulia ni Kaimu Katibu wa shirika hilo, Zuhura Pinde. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Mmoja wa wafanyakazi walioteuliwa na Bodi ya Shirika hilo kukaimu moja ya nafasi zilizowazi ya Meneja Mkuu Menejimenti ya Rasilimali za Shirika, Macrice Mbodo (kuli), akiwa katika mkutano huo. Kushoto ni Mkuu wa Idara ya Usalama ya shirika hilo, George Mwamgabe.
Baadhi ya viongozi wa Shirika la Posta Tanzania wakiwa katika mkutano huo.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania, Dk. Haruni Kondo.
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa kazini wakichukua taarifa hiyo, iliyokuwa ikitolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania, Dk. Haruni Kondo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania, Dk. Haruni Kondo (kulia), akimtambulisha kwa waandishi wa habari, Kaimu Meneja Mkuu Menejimenti ya Rasilimali za Shirika, Macrice Mbodo.
Taarifa kamili ya bodi hiyo kama ilivyowasilishwa na Mwenyekiti wake, Dk. Haruni Kondo jijini Dar es Salaam jana.
SHIRIKA
LA POSTA TANZANIA
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI MKUTANO ULIFANYIKA KATIKA
UKUMBI WA MIKUTANO WA POSTA HOUSE
TAREHE 25 FEBRUARI, 2017
Kwa
kuzingatia maendeleo ya mageuzi makubwa yanayojitokeza katika sekta ya
mawasiliano, Shirika la Posta Tanzania kama mtoa huduma kwa umma (Public Postal
Operator), linawajibika kuhakikisha kuwa huduma za kisasa zinazozingatia vigezo
vya ubora, usalama, uadilifu katika utendaji na uwajibikaji zinawafikia watu
wengi zaidi katika maeneo yote ya nchi.
Kwa
hivi sasa Bodi ya Wakurugenzi pamoja na Menejimenti imechukua hatua katika
maeneo yafuatayo:-
1)
KUPAMBANA NA UHALIFU WA
MADAWA YA KULEVYA.
Shirika
la Posta Tanzania limechukua hatua kadhaa ili kuhakikisha linashiriki na
kuchangia kikamilifu jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano za kupambana na
uhalifu, ikiwa ni pamoja na usafirishaji, uuzaji na utumiaji wa madawa ya
kulevya, usafirishaji na utakatishaji wa fedha haramu, ugaidi, udanganyifu
katika utambulisho pamoja na uhalifu mwingine wa kimtandao wa Kitaifa na
Kimataifa.
Bodi
ya Wakurugenzi ya Shirika imedhamiria kuongeza msukumo na kasi ya usimamizi ili
kupambana na uhalifu huu ambao una madhara makubwa kwa jamii.
Hatua
mojawapo zilizochukuliwa na Shirika ni kusimika mfumo wa kisasa wa kudhibiti
usalama na kurahisisha utambuzi wa vitu na matukio hatarishi na haramu
yanayopitishwa au kujitokeza kupitia mtandao wa Shirika.
Mfumo
huu uliogharimu zaidi ya shilingi milioni mia mbili (200) ambao unajumuisha
ufungaji wa kamera za kiusalama (CCTV) katika Posta Kuu ya Dar es Salaam,
tayari mzabuni aliyeusimika ameshakamilisha kazi yake na ataukabidhi kwa Shirika
wiki ijayo na utazinduliwa rasmi wakati wowote kuanzia hapo.
Aidha,
tumesimika mifumo ya kisasa ya kiusalama ikiwa ni pamoja na mashini za ukaguzi
wa mizigo (baggage scanners) katika Ofisi zenye uwezekano wa kuwa uchochoro wa
uhalifu wa aina hii ikiwa ni pamoja na Ofisi za Zanzibar, Kigoma, Dar es Salaam
na Arusha.
Hatua
hii imechukuliwa kwa kuzingatia kuwa matukio ya uhalifu uliopangwa (organized
crimes) yamekuwa ni changamoto kubwa kwa Mashirika ya Posta Duniani na hivyo
tumedhamiria kuhakikisha kuwa, mtandao wa Shirika wa Kitaifa sio uchochoro wa
uhalifu huu.
Vitu
visivyoruhusiwa kusafirishwa katika mtandao wa Posta kwa mujibu wa sheria ni
pamoja na madawa ya kulevya, bidhaa za kemikali zenye sumu, silaha za moto na
milipuko, wanyama hai, nyara za Serikali, vifaa vya mionzi, vyakula vinavyooza,
betri za aina mbalimbali, vimiminika, fedha haramu, utakatishaji wa fedha na
vitu vyovyote hatarishi.
Katazo
la vitu hivi kusafirishwa katika mtandao wa Posta limezingatiwa katika sheria
na taratibu mbalimbali za Kitaifa ikiwa ni pamoja na sheria ya Mawasiliano ya
Elektroniki na Posta (EPOCA) ya mwaka 2010, Umoja wa Posta Duniani (UPU),
Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga (ICAO) na Shirika la Forodha Duniani
(WCO).
Kwahiyo,
Shirika la Posta Tanzania kwa kushirikiana na vyombo vingine vya usimamizi wa
sheria, kwa hivi sasa limeimarisha uhakiki wa mifumo yake na pia ukaguzi wa
barua, vifurushi, vipeto na mizigo ili kujiridhisha juu ya usalama na
uzingatiaji wa sheria.
2)
UANZISHWAJI WA JAMII
CENTRE
Hatua
nyingine iliyochukuliwa ni uanzishwaji wa kituo cha kisasa cha huduma ya Jamii
Centre katika Posta Kuu ya Dar es Salaam iliyoko mtaa wa Azikiwe.
Maandalizi
ya Ofisi ikiwa ni kaunta za kutolea huduma, mifumo ya mawasiliano, samani kwa
wateja, mafunzo ya wahudumu na vifaa vya kazi tayari vimefungwa ili vitumike na
kituo kiko tayari kwa uzinduzi, wakati wowote kuanzia sasa.
Kituo
kinatoa huduma jumuishi za kimtandao katika sehemu moja (One Stop Community
Centre) ili kuwapunguzia wananchi usumbufu wa kufuata huduma hizo maeneo mbalimbali
tofauti.
Huduma
zinazotolewa ‘on-line’ kwa sasa ni pamoja na:-
Ø Malipo
ya wastaafu (NSSF)
Ø Malipo
ya gawio (dividends) za makampuni mbalimbali
Ø Malipo
ya usajili wa Baraza la Mitihani
Ø Huduma
za kibenki- CRDB
Ø Moneygram
Ø Maxmalipo
(Road lincense), Luku, Ving’amuzi n.k
Ø Huduma
mbalimbali za Posta.
Bodi
imeelekeza Menejimenti kuendelea na ushawishi kwa makampuni na taasisi nyingine
kama RITA, NHIF, NIDA, Mabenki n.k ili kujiunga na mfumo huu wa kisasa. Hapo baadae zichukuliwe hatua za kufungua
vituo vingine katika miji/mikoa ya Zanzibar, Dodoma, Mbeya, Mwanza, Arusha na
Morogoro kabla kufikia mwisho wa 2017.
3)
USIMAMIZI WA KADA ZA
UONGOZI NA RASILIMALI WATU
Baada
ya Bodi kufanya tathmini yake juu ya utendaji wa Wafanyakazi wa Shirika, imeelekeza
Menejimenti ichukue hatua stahiki kwa kada zote za Wafanyakazi kuanzia hapa
Makao Makuu, Zanzibar, Mikoani, Wilayani hadi Vijijini.
Bodi
inatambua kuwa ufanisi wa Shirika hili utatokana na utendaji wa Rasilimali watu
iliyopo. Kwa hivi sasa Shirika lina Wafanyakazi wenye ajira ya kudumu wapatao
1,082 hadi kufikia Disemba 2016 lakini, baadhi yao wanafanya kazi kwa mazoea na
lazima sasa wabadilike.
Menejimenti
iendelee kusimamia uwajibikaji wa Viongozi na Watumishi wa kada zote ndani ya
Shirika ili kujenga nidhamu ya kazi, kujituma, kuheshimu kanuni na taratibu,
kuongeza ubunifu na kufanya kazi kwa ufanisi wenye tija kwa Shirika.
Bodi
inatambua jitihada za Menejimenti za kuwa na mkakati wa kuimarisha usimamizi na
udhibiti wa nidhamu za Wafanyakazi hususani katika kuwaongezea uwezo, kutokana
na mafunzo wanayopewa kulingana na uhitaji wa soko, utii, uaminifu na hamasa
katika utendaji wa kazi.
Ili
kuthibitisha hilo, Wafanyakazi wanapoajiriwa wanakula viapo vya utii na kutunza
siri katika utendaji kazi wao na tunapenda kuendelea kuajiri Wafanyakazi wenye
uwezo na fuzu sahihi ili kuendana na mabadiliko ya soko na Wafanyakazi
waendelee kupewa mafunzo ya mara kwa mara ili kuongeza ufanisi na dhana ya
kumjali mteja.
Aidha,
kwa wakati huu kuna mwelekeo mzuri kwani Shirika limeanza kuwapima Wafanyakazi
kwa kutumia mfumo wazi wa kazi (OPRAS) kwa kuanzia mwaka huu wa fedha
2016/2017, na itakapobainika kuwa wapo Wafanyakazi ambao hawakufikia viwango
vya utendaji lazima wawajibishwe.
Kwa
kuzingatia yote hayo, katika kikao chake cha jana tarehe 24/2/2017 Bodi ilipitia kwa makini
utendaji, uwajibikaji na nidhamu na uwezo wa watendaji wakuu katika Shirika
hilo ambao wanatakiwa kuwa mfano bora wa uongozi wa utendaji mzuri .
Imebainika
na kujiridhisha kuwa baadhi ya watendaji wakuu Makao Makuu ya Posta wamekuwa kikwazo katika dhana
ya uwajibikaji, weledi, na kujituma katika kutekeleza wajibu na majukumu yao
ili kulifanya Shirika la Posta kuwa mfano bora wa Mashirika yenye ubora katika
kutoa huduma.
Aidha,
kuna baadhi ya vitendo kwa baadhi ya watendaji vinadhihirisha tabia ya
umangimeza, urasimu, kufanya kazi kwa mazoea ubadhirifu na wizi.
Bodi
imeamua kufanya mabadiliko ya uongozi wa juu wa Shirika la Posta kwa kutengua
nafasi za watendaji wakuu:
1)
Meneja Mkuu
Menejimenti ya ya Rasilimali za Shirika Ndg. James M. Sando na kumteua Ndugu
Macrice Mbodo kukaimu nafasi hiyo.
2)
Meneja Mkuu
uendeshaji wa Biashara Bi. Janeth Msofe na kumteua aliyekuwa Meneja Mkoa
Shinyanga Ndugu. Hassan Mwang’ombe.
3)
Imemsimamisha kazi
Ndugu. Jasson Kalile aliyekuwa Meneja Msaidizi Mail and Logistic.
4)
Imemsimamisha Kazi
Ndugu Ambrose John aliyekuwa Senior Motor Transport Officer.
IMETOLEWA NA:-
MWENYEKITI
BODI YA WAKURUGENZI
SHIRIKA LA POSTA TANZANIA
DAR ES SALAAM
No comments:
Post a Comment