ANGALIA LIVE NEWS

Friday, February 24, 2017

JESHI LA MAGEREZA NA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII YA NSSF& PPF WAINGIA UBIA RASMI UJENZI WA KIWANDA CHA SUKARI GEREZA MBIGIRI, MOROGORO

Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akitoa maelezo mafupi kabla ya hafla fupi ya utiaji saini wa Mkataba wa Makubaliano kati ya Jeshi la Magereza na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya NSSF & PPF katika ushirikiano wa kufufua Kilimo cha miwa na ujenzi wa Kiwanda cha sukari cha Gereza Mbigiri – Morogoro. Hafla hiyo imefanyika leo Februari 24, 2017 katika Ofisi za Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mtendaji wa Kampuni Tanzu ya Mkulazi ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya NSSF & PPF, Bw. Nicander Kileo (kushoto) na Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(kulia) kwa pamoja wakisaini Mkataba wa Makubaliano(Memorundum of Understanding) kati ya Jeshi la Magereza na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya NSSF & PPF katika ushirikiano wa kufufua Kilimo cha miwa na ujenzi wa Kiwanda cha sukari cha Gereza Mbigiri – Morogoro. Hafla hiyo ya utiaji saini imefanyika leo februari 24, Jijini Dar es Salaam.
Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(kulia) na Kaimu Mtendaji wa Kampuni Tanzu ya Mkulazi ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya NSSF & PPF, Bw. Nicander Kileo(kushoto)wakionesha nyaraka mbalimbali baada ya hafla fupi ya uwekaji saini wa Mkataba wa Makubaliano kati ya Jeshi la Magereza na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya NSSF & PPF katika ushirikiano wa kufufua Kilimo cha miwa na ujenzi wa Kiwanda cha sukari cha Gereza Mbigiri – Morogoro.
Maafisa Waandamizi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya NSSF & PPF wakifuatilia hafla ya uwekaji saini wa Mkataba wa Makubaliano hayo kama inavyoonekana katika picha.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa PPF, Bw. William Erio akizungumza katika hafla fupi ya uwekaji saini wa Mkataba wa Makubaliano kati ya Jeshi la Magereza na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya NSSF & PPF katika ushirikiano wa kufufua Kilimo cha miwa na ujenzi wa Kiwanda cha sukari cha Gereza Mbigiri – Morogoro.
Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakishuhudia uwekaji saini wa Mkataba wa Makubaliano hayo kama inavyoonekana katika picha.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa NSSF, Prof. Godius Kahyarara akizungumza katika hafla fupi ya uwekaji saini wa Mkataba wa Makubaliano kati ya Jeshi la Magereza na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya NSSF & PPF katika ushirikiano wa kufufua Kilimo cha miwa na ujenzi wa Kiwanda cha sukari cha Gereza Mbigiri – Morogoro

Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa Waandandamizi wa Jeshi la Magereza(waliosimama) mara baada ya hafla ya uwekaji saini wa Mkataba wa Makubaliano hayo(wa pili kushoto) ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa PPF, Bw. William Erio(wa pili toka kulia) ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa NSSF, Prof. Godius Kahyarara(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

No comments: