ANGALIA LIVE NEWS

Friday, February 24, 2017

MSHUKIWA MKUU WA MADAWA YA KULEVYA AKAMATWA-BBC

Paul Makonda kamishna wa eneo la Dar es Salaam
Maafisa wa polisi nchini Tanzania wanasema kuwa wamemkamata kiongozi wa ulanguzi wa dawa ya kulevya aina ya heroine anayefanya operesheni zake kati ya Afrika mashariki na China.

Maafisa hao wanaokabiliana na ulanguzi wa mihadarati wanasema kuwa Ayub Mfaume ambaye anajulikana kama kiboko alikuwa mmoja wa watu wanaotafutwa sana nchini humo.

Anadaiwa kuwa na ushiirikiano na walanguzi wa mihadarati nchini Brazil, Pakistan, na mataifa kadhaa ya Ulaya.

Maafisa hao wanasema kuwa Bwana Mfaume alijisalimisha kwa maafisa hao kufuatia msako wa wiki mbili dhidi ya walanguzi wa mihadarati

No comments: