Balozi Amina ambaye alipoteza wadhfa huo kwa mpinzani wake kutoka Chad Moussa Faki Mahamat alilaumu kushindwa kwake kulitokana na uwongo wa majirani za Kenya na siasa zinazoendelea kati ya mataifa yanayozungumza Kifaransa Francophone na wale wanaozungumza kizungu Anglophone.
Akiongea na vyombo vya habari vya kimataifa mjini Addis Ababa Amina alisema kuwa alipoteza wadhfa huo kutokana na usaliti wa majirani za Kenya ambao walikuwa wameunga mkono harakati zake.
''Baadhi ya majirani zetu hawakutuunga mkono, walisikika wakizungumzia swala hilo'', Amina alisema bila ya kutaja majina.Nadhani hofu kwamba pengine Kenya ingeshinda ndio iliowafanya kutotuunga
mkono''.
''Nadhani sisi Wakenya ni watu waaminifu sana kwa hivyo ni vigumu kushirikiana na watu wanaohadaa.kwa hivyo nadhani walijiondoa''.
Tukisonga mbele ni funzo zuri kwetu sisi. Katika raundi ya tano ya kura hizo Amina alikuwa anaongoza kwa kura 27 dhidi ya za Mahmat 25'',aliongezea Amina.
Taifa moja halikupiga kura.
Ni wakati huo ambapo mataifa mawili kutoka shirika la IGAD yaliamua kumpigia kura mpinzani wa Amina na hivyobasi kumpatia kura 28 zaidi ya 26 zilizohitajika ili mgombea kuibuka mshindi.
BBC
1 comment:
Mama ametumia mafumbo kuwashutumu jirani zake. Kwa nini asiwe na guts kuzitaja nchi jirani zilizowasaliti Kenya? Acha umbea mama Amina, tunza hadhi yako. Kwa mtazamo wangu, ilikuwa ni jambo la busara kumchagua a). Mwanaume, vile aliyestaafu uenyekiti alikuwa ni mwanamke ambaye alichaguliwa mara mbili mfululizo. Hivyo ni fair game kumchagua opposite gender. b). Mama Zuma, mwenyekiti aliyestaafu anatoka Afrika Kusini, ambayo ni Anglophone block. It makes sense, to switch around or to alternate for that matter. Jaribu tena next time mama, labda sala zako zitapokelewa.
Post a Comment