Bi Mohammed ambaye alikuwa anapigiwa upatu kushinda wadhfa huo aliyalaumu mataifa ya Afrika mashariki kwa kuihadaa Kenya na kutaka uchunguzi ufanywe.
Vyombo vya habari nchini Kenya vimesema kuwa mataifa ya Uganda, Burundi na Djibout hayakumpigia kura Amina Mohammed katika raundi ya mwisho na hivyobasi kumsaidia mgombea wa Chad Moussa Faki Mahamat kushindwa kiti hicho.
Bw Mahamat alipata thuluthi mbili ,ama kura 36 na kutangazwa mshindi.
Serikali ya Kenya ilidaiwa kutumia dola milioni 3 katika kampeni zake kumpigia debe bi Mohammed.
Kwa kawaida wadhfa huo huzunguka kati ya mataifa yanayozungumza kiingereza Anglophone na yale yanayozungumza kifaransa Francophone.
Mwenyekiti anayeondoka Nkosazana Dlamini Zuma kutoka taifa linalozungumza kiingereza Afrika Kusini alimrithi kiongozi aliyekuwa akizungumza Kifaransa Jean Ping 2012.
Uganda ilisema katika taarifa kwamba ilimuunga mkono Amina Mohammed kabla na hata baada ya uchaguzi huo.
No comments:
Post a Comment