Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga, akipokea vifaa vya kuzuia vumbi kwa askari wa usalama barabarani kutoka kwa msamaria mwema, Tahir Othman (kulia) ,aliyejitolea vifaa hivyo ili kusaidia askari kuepukana na vumbi kuingia kwenye njia ya hewa wawapo katika shughuli zao.Anayeshuhudia katikati ni Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni.Makabidhiano hayo yamefanyika ofisini kwa Naibu Waziri,jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga, akionyesha kwa waandishi wa habari jinsi ya kuvaa kifaa cha kuzuia vumbi kwa askari wa usalama barabarani alivyopokea kutoka kwa msamaria mwema,Tahir Othman(hayupo pichani) ,aliyejitolea vifaa hivyo ili kusaidia askari kuepukana na vumbi kuingia kwenye njia ya hewa wawapo katika shughuli zao.Kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani,Mhandisi Hamad Masauni. Makabidhiano hayo yamefanyika ofisini kwa Naibu Waziri, jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ambaye
pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani,Mhandisi Hamad
Masauni, akiangalia jinsi ya kuvaa kifaa cha kuzuia vumbi kwa askari kutoka kwa
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga,ambae pia ni Katibu
Mtendaji wa baraza hilo.Vifaa hivyo vilitolewa na msamaria mwema,Tahir
Othman(hayupo pichani).Makabidhiano hayo yamefanyika ofisini kwa Naibu
Waziri,jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
No comments:
Post a Comment