Rais John Magufuli, ametunuku kamisheni kwa maofisa 165 wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika vyeo vya Luteni Usu.
Hafla ya kutunuku kamisheni hizo imefanyika leo Ikulu jijini Dar es Salaam ambapo miongoni mwao wanaume ni 143 na wanawake ni 22.
Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli, Meja Jenerali Paul Masao, akizungumza katika hafla hiyo alisema wahitimu wa mafunzo hayo ni pamoja na maofisa 15 kutoka mataifa mengine.
No comments:
Post a Comment