ANGALIA LIVE NEWS

Friday, February 24, 2017

Makonda agoma kuzungumzia kughushi vyeti



Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda
By Elizabeth Edward, Mwananchi

Dar es Salaam. Licha ya kuandamwa na tuhuma za kughushi vyeti, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema hawezi kuzungumzia suala hilo kwani majibu yake yapo mtandaoni sakata lilipoanzia.

Makonda amesema hayo leo (Ijumaa) alipoulizwa swali na wanahabari kuhusu uhakika wa taarifa zinazosambaa mitandaoni kuwa alinunua vyeti na kutumia jina lisilo lake.

"Maswali ya mitandaoni yanaishia mitandaoni siko hapa kupoteza focus (mwelekeo).Ukiona maneno mengi yanaibuka kwenye ishu ya dawa za kulevya ndiyo ujue vita imefika penyewe,"amesema Makonda.

No comments: