ANGALIA LIVE NEWS

Friday, February 24, 2017

Mmoja afariki, sita hawajulikani walipo baada ya boti kuzama Wete

By Haji Mtumwa, Mwananchi hmtumwa@mwananchi.co.tz

Zanzibar. Mtu mmoja amefariki dunia na wengine sita hawajulikani walipo baada ya boti iliyokuwa ikitokea Mombasa, kuelekea Wete, Pemba kupigwa wimbi kali na kuzama huko visiwani Zanzibar usiku wa kuamkia leo.

Mkuu wa Wilaya ya Wete, Rashid Hadidi alisema watu wengine kumi waliookolewa wamepelekwa hospitali ya Wilaya ya Wete, kwa ajili ya matibabu.

“Boti hiyo ya Al Hussein ilizama wakati ikishusha watu karibu na kisiwa cha Oesha na watu kumi waliookolewa wamelazwa katika hospitali ya Wete,” alisema Hadidi

Alisema idadi ya watu waliokuwamo katika boti hiyo ni 27, ambapo kumi ndiyo waliookolewa.

Alisema aliyefariki ni raia wa Mombasa Kenya na bado jina lake halijapatikana.

No comments: