Wanahabari mkoa
wa Iringa walioshiriki warsha ya siku moja ya gesi asilia wakiwa
katika picha ya pamoja na mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela wa
tatu kutoka kushoto na wawezeshaji wa warsha hiyo kutoka
TPDC,warsha iliyofanyika ukumbi wa VETA Iringa kwa kushirikisha
wanahabari kutoka mkoa wa Njombe ,Ruvuma na wenyeji Iringa.
Wanahabari mkoa
wa Njombe walioshiriki warsha ya siku moja ya gesi asilia wakiwa
katika picha ya pamoja na mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela wa
tatu kutoka kushoto na wawezeshaji wa warsha hiyo kutoka
TPDC,warsha iliyofanyika ukumbi wa VETA Iringa kwa kushirikisha
wanahabari kutoka mkoa wa Njombe ,Ruvuma na wenyeji Iringa
Wanahabari mkoa wa Ruvuma walioshiriki warsha ya siku moja ya gesi
asilia wakiwa katika picha ya pamoja na mkuu wa wilaya ya Iringa
Richard Kasesela wa tatu kutoka kushoto na wawezeshaji wa warsha
hiyo kutoka TPDC,warsha iliyofanyika ukumbi wa VETA Iringa kwa
kushirikisha wanahabari kutoka mkoa wa Njombe ,Ruvuma na wenyeji
Iringa
Na Fredy Mgunda,Iringa.
Mkuu
wa Wilaya ya Iringa Mh. Richard Kasesela amelipongeza Shirika la Maendeleo ya
Petroli Tanzania (TPDC) kwa kuendesha mafunzo maalum kwa waandishi wa Habari wa
Mikoa ya Arusha, Iringa,Ruvuma na Njombe ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa mafunzo
ya siku moja ambayo yamefanyika mwezi wa pili tarehe ishirini na moja mwaka
huu(21 / 02 /2017) katika ukumbi wa Chuo cha VETA mkoani Iringa.
“Ingawa mafunzo ni mafupi lakini napenda kulipongeza Shirika letu la Mafuta la
Taifa kwa kuona umuhimu wa vyombo vya habari katika kupata uelewa mpana wa
Sekta Ndogo ya Mafuta na Gesi ili waweze kuhabarisha na kuelimisha watanzania
kwa ujumla ili watambue shughuli za shirika na faida zake haswa katika uchumi
wa nchi”, alieleza Mkuu wa Wilaya.
Aidha Mh Kasesela amewaomba Waandishi wa Habari kuwa wazelendo katika kuisaidia
Serikali kutekeleza miradi mbalimbali yenye maslahi mapana katika maendeleo ya
nchi yetu.
‘’Waandishi Wahabari mnapaswa
kuisaidia Serikali katika utekelezaji wa miradi mbalimbali yenye tija kwa
uchumi wa Taifa, mfano katika vita ya kiuchumi ya kugombania mradi wa bomba la
mafuta ghafi kutoka Uganda kati ya Tanzania na Kenya, wenzetu Kenya
walijitahidi kuandika habari zenye kutoa wasifu wa nchi yao ili kuisaidia
kupata mradi huo, hivi ndivyo mnavyopaswa kufanya kazi kiuzalendo.”
Aliongeza kuwa leo hii mmeweza kuifahamu TPDC sasa mnapaswa kuwaeleza wananchi miradi inayofanywa na Shirirka hili na manufaa yake katika uchumi wa Taifa, mwende mkatafiti namna mradi wa bomba la mafuta utakavyonufaisha wananchi wanaoishi kando ya njia ya bomba hilo, vilevile namna bomba hilo litakavyosaidia kukuza uchumi wa nchi, hivi ndivyo tunavyoweza kujenga nchi yetu kupitia taaluma ya uandishi wa habari.
Kasesela alisisitiza kuwa ili tujenge Taifa imara ni vyema tuandike habari kwa weledi, uzalendo huku tukiondoa tofauti zetu za kiitikadi ziwe za kikabila, kisiasa au kidini kwa namna hii tutaweza kuandika habari zenye kujenga nchi yetu na si vinginevyo.
Alisisitiza vile vile juu ya utoaji
taarifa mapema pale mtu anapoona kuna hujuma au uharibifu wa aina yoyote katika
miundombinu hii, akiongea katika warsha hiyo alisema “miundombinu hii ya gesi
na mafuta ni mali ya watanzania hivyo kuilinda ni jukumu letu sote kama
wazalendo wa nchii hii”.
Akiongea wakati wa ufunguzi wa
warsha hiyo, Afisa mahusiano wa
Shirika la Maendeleo ya Petroli na gesi Tanzania Maria Mselemu alisema
warsha hii inalenga kuendelea kuwajengea uwezo zaidi waandishi wetu wa habari
kuweza kuripoti kwa umahiri na ustadi habari za mafuta na gesi.
Mselemu aliwashukuru waandishi wa habari kwa juhudi zao za kuupasha
habari umma na kuwaasa kwamba kalamu yao ina nguvu hivyo ni vyema ikaendelea
kutumika kujenga uchumi wa Taifa kwa kutoa taarifa sahihi kila wakati.
Katika taarifa yake Faustin Kayombo kutoka mkondo wa juu (TPDC) alisisitiza juu ya matarajio yasiyo halisia yaliyopo miongoni mwa wanajamii na kuwaomba waandishi wa habari kusaidia kuwaeleza wananchi juu ya uhalisia wa sekta.
Kayombo alisema kwamba uwekezaji katika sekta ya mafuta na gesi ni
wa gharama kubwa na hata mafaniko kwa maana ya mapato makubwa kwa Serikali
huchukua muda mrefu kuonekana.
Akitolea mfano mradi mkubwa wa kusindika gesi asilia (Liqufied Natural Gas-LNG), Kayombo alifafanua kwamba itachukua takribani miaka 8 hadi 10 kabla ya mzigo wa kwanza wa LNG kusafirishwa kwenda katika soko la dunia kwa mauzo.
Akitolea mfano mradi mkubwa wa kusindika gesi asilia (Liqufied Natural Gas-LNG), Kayombo alifafanua kwamba itachukua takribani miaka 8 hadi 10 kabla ya mzigo wa kwanza wa LNG kusafirishwa kwenda katika soko la dunia kwa mauzo.
Hata hivyo Kayombo alisisitiza
juu ya ushiriki wa wazawa katika sekta hii hususan katika kutoa huduma na kuuza
bidhaa.
Naye mwanasheria wa TPDC Barnabas Mwashambwa alisema sheria mpya ya
petroli ya mwaka 2015 inawataka wawekezaji wote kutumia bidhaa zinazozalishwa
hapa nchini na kama ikitokea bidhaa hizo hazipo nchini basi kampuni iingie ubia
na kampuni ya kizawa ili kuweza kutoa huduma inayohitajika.
Sheria imeeleza kwamba ubia huo
lazima umpe mzawa ushiriki usiopunguza asilimia 25%, hii ni fursa kwa wazawa na
ni vyema ikachangamkiwa.
Hata hivyo Mwenyekiti wa Waandishi wa Habari mkoa wa Iringa frank leornad ameliomba Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kutenga muda wa kutosha zaidi katika uelimishaji ili walengwa waweze kuelewa vyema sekta, ombi ambalo liliungwa mkono na Mkuu wa Wilaya.
Katika mafunzo hayo waandishi wa habari walipata fursa ya kujifunza kuhusu maendeleo ya Sekta Ndogo ya Mafuta na Gesi, Matumizi ya Gesi Asilia na Faida Zake, Mradi wa Bomba la Kusafirisha Mafuta Ghafi kutoka Uganda hadi Tanga na Usambazaji wa Gesi Asilia Majumbani, Viwandani na kwenye Vituo vya Kujaza Magari.
TPDC
imeendelea kutoa elimu kwa wadau mbalimbali ikiwa na lengo la kuongeza uelewa
zaidi katika sekta hii mpya na changa ya mafuta na gesi hapa nchini.
No comments:
Post a Comment