ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, February 5, 2017

MKAZI WA MARYLAND NCHINI MAREKANI AMUUA BINTI YAKE KWA KUTOPIGA MSWAKI

Image result for IRIS HERNANDEZ-RIVER (20)
IRIS HERNANDEZ-RIVER (20) pichani juu anayeishi Gaithersburg kaunti ya montgomery anashikiriwa na Polisi baada ya kumuua bintie Nohely Alexandra Martinez Hernandez wa miaka minne kwa kumpiga teke tumboni na mwanae kuangukia kichwa.

IRIS HERNANDEZ-RIVER alichanganyikiwa na ilimchukua zaidi ya saa moja kabla hajapiga simu ya 911 ili kupata msaada wa Hospitali baada ya mwanae kupelekwa huko akiwa mahututi na baadae mtoto hyo aliga Dunia.

Msemaji wa Polisi amesema tukio hilo la kusikitisha lilitokea mwishoni mwa mwezi Januari tarehe 26, 2017 na mwanae kuaga Dunia Jumatano iliyopita kutokana na kipigo hicha cha mama yake.

IRIS HERNANDEZ-RIVER aliiambia polisi mwanae aliingia bafuni kuoga kwenye saa 5:15 asubuhi na baadae mama mtoto alimkuta mwanae kichwa chini kwenye sinki la kuogea na ilimchukua zaidi ya saa moja kupiga simu kuomba msaada wa huduma ya kwanza na mwanae kupelekwa hospitali akiwa mahututi.

No comments: