Farmajo alipata kura 184, Bw Hassan Sheikh akapata kura 97 naye rais mwingine wa zamani Sharif Sheikh Ahmed akapata kura 46.
Mshindi alitakiwa kupata thuluthi mbili ya kura zote zilizopigwa lakini kabla ya duru ya tatu kufanyika, Bw Hassan Sheikh alikubali kushindwa na kumpongeza Farmajo.
Farmajo alihudumu kama waziri mkuu nchini Somalia mwaka 2010 na 2011.
"Huu ni ushindi wa Somalia na kwa Wasomali," Farmajo aliwaambia wabunge waliokusanyika katika ukumbi ulio katika uwanja wa ndege Mogadishu, ambao ndio waliomchagua.
Aliapishwa kura rais muda mfupi baadaye.
Baada ya habari za ushindi wake kuanza kuenea, milio ya risasi ilisikika pande mbalimbali za Mogadishu, watu wakisherehekea ushindi wake.
Mwanamke wa kwanza kutangaza kuwa angewania urais nchini Somalia ingawa alijiondoa baadaye, Fadumo Dayib ameonekana kufurahia ushindi wa Farmajo.
Ameandika kwenye Twitter: "Wabunge bila shaka wamechagua chaguo la wananchi. Wameiokoa Somalia!! Kumepambazuka, ni mwanzo mpya!"
Taifa la Somalia linalokabiliwa na vita vya kikabila pamoja na vile vya ukoo halijafanikiwa kufanya uchaguzi wa kidemokrasia unaoshirikisha raia kushiriki katika uchaguzi tangu 1969.
Uchaguzi huo ulifuatiliwa na mapinduzi, uongozi wa kiimla na vita vya wenyewe kwa wenyewe vinavyoshirikisha koo na wapiganaji wa al-Shabab.
Uchaguzi huo unaonekana kama mojawapo ya harakati za kujenga tena demokrasia mbali na kuweka uthabiti.
Matokeo ya duru ya kwanza
Hassan Sheikh Mohamud - 88 (rais aliyeondoka)
Mohamed Abdullahi Mohamed "Farmajo" - 71 (waziri mkuu wa zamani)
Sharif Sheikh Ahmed - 49 votes (rais wa zamani aliyemtangulia Hassan Sheikh)
Omar Abdirashid A. Sharmarke - 38 (waziri mkuu anayeondoka)
BBC
No comments:
Post a Comment