Shelia Fedrick ameyafahamisha hayo, vyombo vya Habari nchini Marekani
Mhudumu wa ndege aeleza alivyomhudumia mhasiriwa wa utumwa wa binadamu.
Wakati Shelia Fedrick alipomuona msichana mchafu na aliye na nywele ambayo haijachanwa, akiwa ameketi karibu na mzee mmoja wa kiume alikuwa amevalia nadhifu, kwenye ndege, alitaka kujua zaidi.
Msichana huyo chipukizi "alionekana kana kwamba alikuwa amepitia kuzimu", mhudumu huyo wa ndege ameiambia runinga ya NBC huku akiongeza kuwa "mtu huyo hakutaka nizungumze na binti huyo". Alisema Shelia.
Bi Fedrick alimuachia msichana huyo kijikaratasi chenye ujumbe ndani ya choo cha ndege- ili kumfanya msichana huyo aeleze ikiwa anahitaji msaada.
Alimuachia ujumbe huo kwenye kioo, ambaye "aliandika kwenye kijikaratari hicho kwamba anahitaji msaada" Bi Fedrick aliiambia 10News.
Ilibainika baadaye kuwa msichana huyo alikuwa mhasiriwa wa ulanguzi wa watu- na hisia za Bi Fedrick zilisaidia kuokolewa kwake.
Rubani alisaidia kuwafahamisha polisi, waliofika na wakasubiri pale ndege hiyo ilipotua.
Kisa cha mwaka 2011 katika ndege ya Alaska Airlines, kiliripotiwa katika vyombo vya habari wiki hii, huku mabalozi wa kujitolea wa huduma za ndegewalipoanza kuwapa mafunzo wafanyikazi, kuhusu namna ya kukabiliana na biashara haramu ya watu.
Mtandao wa mambalozi hao wa huduma za ndege, wanasema kuwa, wahasiriwa wa biashara ya utumwa wa watu, bila shaka ni waoga kuwajulisha walinda usalama, hawafahamu wanakokwenda na pia ni waoga.
Kwa sasa binti huyo anasoma chuoni, na amekuwa akiwasiliana na Bi Fedrick. Hiyo ni kwa mjibu wa taarifa ya 10 News.
Kwa mjibu wa simu za idara ya taifa ya kupambana na biashara haramu ya ulanguzi wa binadamu, visa 7,572 vya biashara ya watu viliripotiwa nchini Marekani, mwaka 2016.
chanzo:BBC
No comments:
Post a Comment