Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (Kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Mkandarasi wa kampuni ya Sumitomo Mitsui Eng. K Tsuji, anayejenga barabara ya juu (TAZARA fly over) wakati alipokagua maendeleo ya ujenzi huo jijini Dar es salaam.
Mkandarasi wa kampuni ya Sumitomo Mitsui Eng. Mitsui Eng. K Tsuji, (Wa pili kulia) akifafanua jambo kuhusu ramani ya ujenzi wa barabara ya juu (TAZARA fly over) kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (Wa tatu kulia) wakati alipokagua maendeleo ya ujenzi huo jijini Dar es salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (Katikati), akikagua maendeleo ya Ujenzi wa barabara ya juu (TAZARA fly over), jijini Dar es salaam.
Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akisalimiana na baadhi ya
mafundi wanaojenga barabara ya juu (TAZARA fly over), jijini Dar es salaam.
Picha
na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amemtaka Mkandarasi wa kampuni
ya ujenzi ya Sumitomo Mitsui anayejenga barabara ya juu (Fly over) ya Tazara
kuongeza kasi ya ujenzi huo ili kupunguza
muda wa ujenzi wa mradi huo.
Akizungumza katika
eneo la ujenzi huo leo jijini Dar es salaam, Profesa Mbarawa amepongeza hatua
iliyofikiwa sasa lakini pia amesisitiza kuongeza kasi ya ujenzi wa mradi huo
ili wananchi waweze kunufaika.
“Hakikisheni badala ya
kutumia miezi 35 kujenga mradi huu, mnatumia miezi pungufu zaidi ili
kuwawezesha wananchi na wadau wengine kunufaika na fursa za mradi huu”,
amesisitiza Waziri Mbarawa.
Aidha, Amewataka
wafanyakazi wote katika mradi huo kufanya kazi kwa bidii na uaminifu mkubwa kwa
kuwa Serikali ina mpango mwengine wa kujenga Fly over kama hiyo itakayowawezesha
kupata tena fursa ya ajira.
Hatua hiyo itapelekea
kuwezesha wananchi kunufaika na mradi huo mapema, hivyo kupunguza gharama
wanazozipata kutokana na msongamano wa magari uliopo sasa jijini Dar es salaam.
Naye, Balozi wa Japan
nchini Bw. Masaharu Yoshida, amemhakikishia Waziri huyo kuwa ujenzi wa mradi
huo utamalizika kwa wakati na kwa viwango vilivyokusudiwa, hivyo kuondoa
changamoto ya msongamano katika barabara ya Nyerere na Mandela.
Kwa upande wake,
Mkurugenzi wa miradi kutoka Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Eng. Crspinius
Ako, amesema kati ya nguzo 66 zinazohitajika kwenye awamu ya kwanza ya ujenzi
huo, tayari nguzo 43 zimeshasimikwa ardhini, hali itayopelekea ujenzi huo
kwenda kwa kasi.
Mpaka sasa mradi huo
uliozinduliwa tarehe 1 Disemba 2015 umekamilika kwa asilimia 25.3 na zaidi ya
shilingi bilioni 96.5 zinatarajiwa kutumika katika ujenzi wa mradi huo ambao
utakamilika mwezi Oktoba mwaka 2018.
Imetolewa
na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano.
No comments:
Post a Comment