Dar es Salaam. Rais John Magufuli amempongeza Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Ernest Mangu kwa kuwasimamisha kazi askari 12 ili kupisha uchunguzi kwa tuhuma za kujihusisha na biashara za dawa za kulevya.
Jumamosi iliyopita, IGP Mangu aliwasimamisha askari waliotajwa kwenye orodha aliyoitaja Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda wakati akizungumza na wanahabari hivi karibuni juu ya biashara hiyo.
Rais Magufuli ametoa pongezi hizo leo Ikulu jijini hapa wakati wa sherehe za kumuapisha Mkuu mpya wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo.
Amesema hatua aliyochukua IGP Mangu inaleta taswira nzuri kwa Jeshi la Polisi katika vita dhidi ya dawa za kulevya.
1 comment:
SERIKALI YETU INAUMIZA KAZI BILA SHERIA .
UMEMKAMATA NA MADAWA AU NDO ORODHA ULOPEWE TU.
WANATUMIA VYEO KAMA FIMBO HAIKO HIVYO.
NIMESOMA MAMBO YA WATUMIAJ WA MADAWA SWEDEN NA NAJUA WANA HAKI GANI KATIKA JAMII.
MADAWA SIO CHUMVI USEME UKIMWI MTU KULA ANACHA KWA DAKIKA.
INAHITAJI
MA PSYCHOLOGY
TERAPY
PSYCHOTHERAPY NK
NDO UMWONE MTU KTK JANGA.
JELA YENYE WE KUNA WATUMIAJ BANGING NA BANGING HAIUZWI JELA.
TANZANIA TUJIPANGE
WENYE VYEÖ USITUME KISA UNAZIPIKA KISASA TU.
WAWAKAMATE WAUZAJI WAKO MPK WATOTO WA VIGOGO TUNA .
UNATANGAZA VITA WAKATI ALOBEBA SILAJA UNAMWAGOPA.
Post a Comment